Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo Mhe. Leph Benjamini Gembe akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB Business Club ndani ya Mji wa Ifakara. NMB Business Club inawakusanya wafanyabiashara wote wanaowezeshwa na NMB kwa lengo la kuwaendeleza kibiashara. Business Club hii itakuwa ya 33 kuzinduliwa katika mikoa tofauti nchini kusudi likiwa kuwaunganisha wafanyabiashara wote nchini waweze kufaidika na huduma za NMB, Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Bw. Nazareti Lebbi akishuhudia uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombelo Mhe. Leph Benjamini Gembe akifurahia uzinduzi rasmi wa NMB Business Club ndani ya Mji wa Ifakara. NMB Business Club inawakusanya wafanyabiashara wote wanaowezeshwa na NMB kwa lengo la kuwaendeleza kibiashara. Business Club hii itakuwa ya 33 kuzinduliwa katika mikoa tofauti nchini kusudi likiwa kuwaunganisha wafanyabiashara wote nchini waweze kufaidika na huduma za NMB, kwanza kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Bw. Nazareti Lebb na kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Ifakara Bw. William Kaitira.
Hii ni Business Club ya 33 kuzinduliwa na NMB ambapo nyingine ziko katika mikoa tofauti nchi nzima, na kuna mpango wa kuongeza moja zaidi kabla ya mwisho wa maka. Dhumuni kubwa ni kuwaunganisha wafanyabiashara wote nchini waweze kufaidika na huduma za NMB ambazo pia zitawawezeshakujikimu kimaisha. Hadi sasa NMB Business Clubs zina zaidi ya wafanyabiashara 10,000 waliojiunga.
0 comments:
Post a Comment