Benard Mwakyembe, Kaimu Mwenyekiti wa Dar es Salaam kubwa(Great Dar es Salaam)ya Chadema amesema kuwa utumbuaji wa majipu mbele ya umma ni kinyume na taratibu za uongozi akitaja mfano wa kusimamishwa kazi hazalani kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe sio utaratibu nzuri kwani angiitwa na kuchuunguzwa“Ingawa ni vema kuwawajibisha viongozi wazembe lakini Rais anafanya maamuzi kwa mzuka wa ushabiki wa watu pasi nakufuta taratibu za uongozi”amesema Mwakyembe.
Mwakyembe amesema kuwa nyuma ya pazia la utumbuaji majipu kuna majipu makubwa ambapo utaratibu wa kuhojiwa kwa waliotumbuliwa utafanya kupatikana kwa mizizi ya majipu hayo.
“Nyuma ya Wilson Kabwe kuna Mstahiki Meya aliyemaliza Muda wake ambaye ni Didas Masaburi naye alipaswa kuwajibishwa kama mtuhumiwa kutokana na kuwa yeye ni mtu wa pili kusaini mikataba yote ya Jiji .
Na madiwani wote aliohusika na viongizi wote wa serikali wawajibishwe” amesema Mwakyembe.
Aidha alisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha Magufuli kutumia kumbagua Meya wa Jiji la katika ufunguzi wa daraja la Julius Nyerere maarufu kama daraja la Kigamboni baada ya kumfanya awe kama mvamizi kwenye uzinduzi huo.
Henri Kileo Katibu Mkuu Dar es Salaam Kubwa amesma kuwa Mkuu wa Mkoa ni kinara wa vitendo vya ubaguzi wa viongozi wa upinzani ili kuwadhoofisha .
Kadhia hiyo ya ubaguzi imehusishwa pia kwa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kutorusha matangazo au habari inayowahusu wapinzani.
Katibu Mkuu wa Great Dar es Salaam, alisema siku ya uzinduzi wa daraja hilo Mstahiki Meya alipokuwa anahutubia baada ya kupewa nafasi TBC walizima matangazo.
Mwakyembe anasema kuwa kwa shirika hilo kutorusha matangazo ya vyama vya upinzani sio mara ya kwanza kwani wao hawarushi matangazo ya aina yoyote yale yanayowalenga wapinzani
“ikiwa ile ni chombo cha habari cha taifa kinochoendeshwa kwa kodi za wananchi lakini wanahubiri ubaguzi ikiwa na vyama navyo ni vya walipa kodi vilivyosajiliwa kwa mujibu wa katiba.
Kama wanataka iwe hivyo basi waifanye TBC iwe kama Radio Uhuru ya CCM wananchi wajue kwamba ni shirika la utangazaji la CCM” amesema Mwakyembe.
Chanzo;Mwanahalisionline