Home » » WAKUU WA MIKOA WAPYA NA MABALOZI WALIOAPISHWA LEO IKULU DAR ES SALAAM,HAWA HAPA

WAKUU WA MIKOA WAPYA NA MABALOZI WALIOAPISHWA LEO IKULU DAR ES SALAAM,HAWA HAPA


v18

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Nov 05 amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa na kuwahamisha wengine sita na watatu wengine kupangiwa kazi nyingine
.
Wakuu wapya wa Mikoa hao ni pamoja na Bi. Halima Omari Dendego ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Bi. Amina Juma Masenza ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye nae amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni pamoja na Bwn. Magesa S. Mulongo ambaye atakua Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha,Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma,Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi,Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Wengine walioapishwa leo Ikulu ya Dar es salaam na Rasi Jakaya Kikwete ni pamoja na mhe Samwel William Shellukindo kuwa balozi na msaidi wa rais masuala ya diplomasia,Dkt Yohana Budeba kuwa katibu mkuu wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi,Injinia Mbogo Futakamba kuwa katibu mkuu wizara ya maji
.
Mbali na hao pia wengine ni Dkt Donan Mmbando kuwa katibu mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii,Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa balozi wa tanzania nchini Canada pia Mhe Charles Pallangyo kuwa katibu tawala wa mkoa wa geita na Bw Adoh Stephen Mapunda kuwa katibu tawala wa mkoa wa arusha.

v17
v16
v15
v14
v8
v10
v11
v13Picha:issamichuzi.blogspot.com
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger