Katika kikao cha Bunge kilichokaa leo Novemba 26 Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe waliwasilisha Ripoti ya ishu ya Escrow ambapo kama hukupata kusikiliza wakati Ripoti hiyo ikiwasilishwa hii ni sehemu ya uwasilishwaji wa Ripoti hiyo.
“…Katika
fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki hizi yapo majina ya
viongoozi wa kisiasa, viongozi wa madhehebu ya dini, Majaji na
watumishi wengine wa Serikali..“– Zitto Kabwe.
Kwa upande
wa Viongozi wa Kisiasa walioingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi
ni; Mheshimiwa Andrew Chenge Mbunge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti,
shilingi Bil. 1.6, mheshimiwa Anna Tibaijuka Mbunge na Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, shilingi Bil. 1.6, Mheshimiwa William
Ngeleja Mbunge na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, shilingi
milioni 40.4, ndugu Daniel Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na
Madini shilingi milioni 40.4, ndugu Paul Kimiti, ambaye ni Mbunge
mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4 na ndugu Enos
Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCo aliingiziwa shilingi
milioni 161.7…“– Zitto Kabwe.
Kwa upande wa Viongozi wa madhehebu ya Kidini walioingiziwa fedha ni Askofu Methodius Kilain shilingi Milioni 80.9, Askofu Nzigirwa milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Simon milioni 40.4..”– Zitto Kabwe.
“… Kamati
imependekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara
moja na kisha afikishwe Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi
yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha za umma…“– Deo Filikunjombe.
Kwa upande wa Waziri Mkuu kuhusiana na suala hili baada ya kupitia vielezo vilivyomo kwenye ripoti ya CAG
kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa Waziri Mkuu alikuwa ana
taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchota fedha kwenye
akaunti ya Escrow, ushahidi ulioletwa mbele ya kamati za ofisi ya CAG ulionyesha
kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa juu ya jambo hili na kamati
imethibitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua yoyote kuzuia
mhamala huu usifanyike…“– Deo Filikunjombe.
Kamati kwa
kuzingatia kielelezo namba 22 inathibitisha kwamba bila shaka Waziri
Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri sana na kwamba aliridhia mhamala
huu usifanyike, ndio maana katika maelezo yake ya Bungeni mara kadhaa
Waziri Mkuu alilithibitishia Bunge kuwa fedha za ESCROW hazikuwa fedha za umma…”– Deo Filikunjombe.
Kumsikiliza Zitto Kabwe akiwasilisha Ripoti hiyo, bonyeza play hapa
0 comments:
Post a Comment