Matukio ya mimba za utotoni yamekuwa yakijitokeza kila kukicha yakiwa na sura tofauti, mengi yametajwa kuharibu maisha na kupoteza ndoto za wasichana wengi.
Kutoka Nigeria Mzee mwenye umri wa miaka 75 anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13.
Mzee huyo Pa Alabi ambaye ni fundi seremala aliombwa na binti huyo kumtengenezea kiboksi cha kuhifadhia pesa zake, baada ya kumpa kiboksi hicho akaanza kumtongoza na kujenga ukaribu nae hadi binti akakubali.
“..Siku
yenyewe nilimwelezea hisia zangu na akaahidi kulifikiria suala hilo na
baadae akakubali, tulikutana kimwili pale nilipomuomba na tulikuwa
tukiheshimiana, ghafla akaacha kuja kwangu baada ya siku tano baada ya
ile siku ya kwanza tulipokutana kimwili. Siku moja akaja na kuniambia
Bibi yake alimwambia ni mjamzito ndipo alipoacha kuja kwangu na
sikumuona tena hadi Polisi walipokuja kunikamata..”– Pa Alabi.
Siku ya kwanza msichana huyo kukutana na Alabi
alimpatia hela Naira 200 na kumnunulia simu ya mkononi yenye thamani ya
Naira 150 pesa za Nigeria na baada ya kukamatwa na kuhojiwa alijitetea
kuwa hakujua kama ni kosa kukutana kimwili na binti huyo mdogo na
kueleza kuwa lengo lake ilikuwa ni kumuoa na kumtunza yeye na mtoto
wake.
0 comments:
Post a Comment