Home » » AFCON 2015 KUENDELEA KAMA ILIVYOPANGWA

AFCON 2015 KUENDELEA KAMA ILIVYOPANGWA

 

Confederation_of_African_Football_logo.svg_-1024x953
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeamua kutosogeza mbele michuano ya kombe la mataifa ya Afrika itakayofanyika mwaka 2015 baada ya kamati yake kuu kukaa hii leo na kufikia maamuzi hayo.
Likitumia mtandao wa kijamii wa twitter , shirikisho hilo limesema kuwa wajumbe wote wa kamati kuu kwa pamoja walifikia uamuzi wa kutohamisha tarehe za michuano hiyo ambazo sasa zitabaki kuwa Januari 17 mpaka Februari nane .
Wakati hayo yakiendelea CAF pia imewapa wenyeji Morocco siku tano za kufanya maamuzi ya kuendelea kuwa wenyeji ama kujitoa na inatarajia kupata uthibitisho toka kwa viongozi wa taifa hilo ifikapo jumamosi ya wiki hii .
Morocco imetishia kujitoa kama mwenyeji wa michuano ya AFCON kwa mwaka 2015 endapo CAF haitaahirisha michuano hiyo kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola .
CAF imezingatia ukweli kwamba ni taifa moja pekee kati ya mataifa matatu yaliyozuiliwa kuandaa matukio yoyote ya michezo ambalo lina nafasi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2015.
Taifa hilo ni Guinea ambao kwa pamoja na Liberia na Sierra Leonne wamezuiwa kuandaa michezo ya kimataifa kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo hatari .
Cha kushangaza toka Morocco ni jinsi ambavyo mamlaka za taifa hilo zimeruhusu Guinea kucheza michezo yake ya nyumbani nchini Morocco na hadi sasa Guinea wamecheza mechi mbili za kufuzu michuano ya AFCON nchini humo .
Endapo Morcco wataamua kujitoa kama wenyeji wa michuano ya AFCON fursa hiyo huenda ikaangukia kwa Ghana au Misri yakiwa mataifa pekee ambayo yameonyesha wazi kuwa na dhamira ya kuandaa michuano hiyo kwa dharura .
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger