Timu ya Swansea city imeendeleza ubabe mbele ya vilabu vikubwa vya ligi kuu ya Uingereza.
Wakicheza kwenye uwanja wao wa Liberty Stadium Swansea city ambayo iliwafunga 2-1 Man United kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi hiyo,Leo Wamefanikiwa kuifunga Arsenal 2-1.
The Gunners walianza kupata goli la kuongoza kupitia mchezaji wao nyota Alexis Sanchez katika dakika ya 63, lakini yule yule mchezaji aliyewaliza Man United Gylfi Sigurdsson akaisawazishia Swansea katika dakika ya 74.
Akitokea benchi Mshambuliaji Bafetimbi Gomez alifunga goli la ushindi dakika mbili kabla ya mechi kuisha na kupelekea jahazi la Arsene Wenger na vijana wake kuzama.
Mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Swansea City 2-1 Arsenal na kuwafanya vijana wa Wenger kushuka kwenye msimamo kwa nafasi moja.
ANGALIA MSIMAMO WA LIGI UIENGEREZA JINSI ULIVYO BAADA MECHI ZA LEO
0 comments:
Post a Comment