Mchungaji wa kanisa la moraviani ushirika wa jakaranda akiongea na waandishi wa habari
Baadhi
ya Wachungaji na Waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi
Oktoba 10 majira ya saa 11 jioni walifunga ofisi zote za Makao makuu ya Kanisa
hilo zilizopo Jacaranda Jijini Mbeya na kumzuia aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo
Mchungaji Nosigwe Buya kuhama kwenye eneo hilo kwenda nyumba nyingine eneo la
Saba saba.
Aliyeyeongoza
zoezi hilo ni pamoja na Frank Phili Mtunza hazina wa Kanisa la Moravian
Ushirika wa Bethelehem ulioko Mama John Jijini Mbeya akiwa na Mchungaji
Mwilgumo pamoja na Mchungaji Mwakyoma.
Ofisi
zilzofungwa kwa kutumia minyoro na mbao ni pamoja na ofisi ya Askofu Alinikisa
Cheyo,Ofisi ya Katbu Mkuu,Ofisi ya Mtunza Hazina Mkuu na lango kuu la kuingilia
makao makuu ya Kanisa hilo.
Hatua
hii ya kufunga ofisi za Kanisa ni la pili kwa mwaka huu awali ilikuwa mwezi
Julai mwaka huu ambapo waumini hao walifunga hivyo hivyo kabla ya Serikali
kuingilia kati na kufanya suluhishi kupitia Kamati ya ulinzi na Usalama ya
Wilaya na kuweka makubaliano.
Hata
hivyo Phili alidai maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama
hayakutekelezwa ikiwa ni pamoja na kumrudisha kazini Mchungaji Nosigwe Buya na
kuacha kumhamisha kituo cha kazi.
Aidha
waumini hao walichukua hatua ya kuzuia kuhamishwa kwa Mchungaji Buya ambapo
alikuwa amefunga mizigo yake huku mkewe akishindwa kupika na kuwahudumia watoto
kwa siku nzima na banda la mifugo limeezuliwa na mtu aliyetumwa kutoka ofisi
kuu.
Pamoja
na juhudi za Kanisa kujaribu kumhamisha Mchungaji Nosigwe Buya ziligonga ukuta
baada ya waumini hao wasiozidi ishirini kumuondoa kijana aliyekuwa akiondoa
mabati na mabanzi ya banda la mifugo kuondoka mara moja na kumtaka mke wa
Mchungaji Buya Edda Kabuka kuendelea na shughuli zake.
Kwa
upande wake Mchungaji Buya alisema kuwa hapingi kuondoka katika nyumba hiyo na
kukataa kwenda kituo kingine cha kazi lakini ameshangazwa na kwenda kinyume na
makubaliano ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya lakini kukiukwa maazimio
ya yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu.
Pia
alidai mgogoro huu umeligawanya Kanisa na kwamba hivi sasa mahubiri
yanayofanyika kanisani yamekuwa ya kutupiana maneno kwa pande mbili
zinazopingana na kufanya waumini kushindwa kupata ufumbuzi wa kudumu na kudai
kuwa suluhu pekee iwe ni kuitisha mkutano mkuu wa Kanisa(Sinodi).
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema amesikitishwa na pande hizo
zinazopingana na kwamba ni kwa nini mgogoro huo haupati ufumbuzi licha ya
Kamati ya ulinzi na usalama kusuluhisha na kwamba Jeshi la Polisi litamkamata
yeyote atakayevunja amani kwani kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa
Raia na mali zake.
Credit na mbeya yetu |
0 comments:
Post a Comment