Home » » SHEIKH PONDA AHACHIWA HURU......HAPELEKWA MAHABUSU KWA KOSA LA UCHOCHEZI

SHEIKH PONDA AHACHIWA HURU......HAPELEKWA MAHABUSU KWA KOSA LA UCHOCHEZI


 



    Sheikh Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu.



    Wakili wa Sheikh Ponda, Bw Juma Nassoro akizungumza jambo na mteja wake mahakamani hapo. 



    …. Nassoro akiteta jambo na Sheikh Ponda.



    Askari akidumisha ulinzi mahakamani hapo.



    Sheikh Ponda  akitoka nje ya Mahakama Kuu baada ya kushinda Kesi ya Ardhi iliyokuwa ikimkabili kisha kurudi mahabusu katika gereza la Segerea.



    ….akipanda Karandinga  la magereza.


    Sheikh Ponda akiwa ndani ya gari la magereza tayari kwa kurudi rumande.

    MAHAKAMA  Kuu ya Tanzania imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda baada ya kuona hana hatia dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self  iliyokuwa inamkabili.

    Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema baada ya kupitia vifungu vyote mahakama imejiridhisha na kuona Sheikh Ponda hana hatia yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa rumande akisubiri kesi nyingine ya madai ya uchochezi,  Mkoani Morogoro inayomkabili.

    Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

    0 comments:

     
    Supported by AMAGA Media services : | |
    Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
    Templete Designed by Abdallah Magana
    Proudly powered by Blogger