Raia wa Tunisia katika zoezi la upigaji kura
Wananchi wa Tunisia leo wanapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Rais tangu kutokea vuguvugu la mapinduzi mwaka 2011.
Mapinduzi hayo yalisababisha vuguvugu hilo la mabadiliko kutabakaa katika nchi nyingine za Kiarabu.
Miongoni
mwa wagombea katika kinyang'anyoro hicho ni mwanasiasa mkongwe Beji
Essabsi, aliyewahi kushika nafasi muhimu wakati wa utawala kabla ya
kutokea mapinduzi.
Bwana
Beji Caid Essabsi anayepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo
ameahidi kurejeha kiwango cha juu cha utulivu wa kisiasa na kiuchumi.
Mpinzani
wake wa karibu ni Rais wa mpito wa sasa Moncef Marzouki ambaye amejenga
jina lake kama mpigania haki za binadamu na kama msimamizi wa moyo wa
mapinduzi na anayetamani mabadiliko. Waziri wa Ulinzi wa Tunia Ghazi
Jeribi amesema ana matumaini nchi itasonga mbele kidemocrasia
Credit BBC
0 comments:
Post a Comment