Ponda akiingizwa kwenye basi la wafungwa kwa ajili ya kwenda Segerea.
Magari ya Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) yakiwa yametanda eneo la mahakama
.
Askari wakiongoza msafara.
Wafuasi wa Ponda wakiimba nyimbo mbalimbali nje ya mahakama.
Dola ikifanya mawasiliano kuimarisha ulinzi.
Ukaguzi mkali kwa kutumia kifaa maalumu ukifanyika katika mlango wa kuingilia Mahakama Kuu.
MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana imetupilia mbali rufaa ya Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda iliyopelekwa
na wakili wake Juma Nassoro ya kupinga hatia ya adhabu aliyohukumiwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidai kuwa hapakuwa na ushahidi
wa kutosha wa kumtia hatiani kwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.
Kesi
nyingine ya uchochezi inayomkabili kiongozi huyo katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu ambayo inasikilizwa na Jaji Augustine Shangwa
imeahirishwa hadi Novemba 20, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment