Home » » KASEKE HAUMIZA VICHWA VIONGOZI YANGA NA SIMBA.

KASEKE HAUMIZA VICHWA VIONGOZI YANGA NA SIMBA.

 Deus Kaseke mwenye jezi ya Zambarau ameziingiza vitani Simba na Yanga zinazowania kumsajili.
4
  .
Kaseke aliingia jijini Dar-es-salaam wiki hii ambako aliletwa na viongozi wa Simba ambao walianza kufanya naye mazungumzo .

Kaseke alikubali kujiunga na Simba kwa sharti la kulipwa ada ya uhamisho ya shilingi milioni 40 huku Simba wakiwa tayari kutoa milioni 20 .

Deus Kaseke mwenye jezi ya Zambarau ameziingiza vitani Simba na Yanga zinazowania kumsajili.

Deus Kaseke mwenye jezi ya Zambarau ameziingiza vitani Simba na Yanga zinazowania kumsajili.
Sinema hii ya kumsajili Kaseke iliingia kwenye hatua tamu zaidi baada ya kuwepo kwa ripoti ya mchezaji huyo ‘kutekwa’ na watu wa Yanga ambao walikuwa wanataka kumsainisha mchezaji huyo kwenye klabu yao .

Kaseke hadi sasa amerudi nyumbani kwao huko Mbeya na timu yoyote itakayokuwa na nia ya kumsajili italazimika kufunga safari na kumfuata huko .

Kumpoteza Deus Kaseke kutakuwa pigo kubwa kwa Mbeya City .

Kumpoteza Deus Kaseke kutakuwa pigo kubwa kwa Mbeya City .
Taarifa nyingine zinadai kuwa Yanga imemtuma mchezaji wake wa zamani ambaye ni kiongozi kwenye klabu hiyo kwenda jijini Mbeya kukamilisha mazungumzo ya usajili wa Deus Kaseke .


Endapo Mbya City itampoteza Kaseke huenda ikawa hatarini kuendelea na mfululizo wa matokeo mabaya ambayo wamekuwa wakiyapata kwani hakuna asiyefahamu kuwa mchezaji huyo ni muhimu kwa klabu hiyo .
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger