SPIKA wa Bunge-Anne Makinda, amelazimika kulihairisha Bunge kwa dharura hadi hapo baadaye kutokana na wabunge wa upinzani kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutaka Serikali itoe ufafanuzi kuhusu uandikishaji wa wapiga kura kwa mfumo wa BVR unaoendelea…Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kizaazaa hicho kiliibuka baada ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) kuomba mwongozo wa Spika akitaka Bunge lisitishe shughuli zake na kujadili suala hilo la dharura kwa sababu hadi sasa hakuna mkoa uliomaliza kuandikisha wapigakura na hivyo kuleta utata kuhusu kura ya maoni ya katiba pendekezwa iliyopangwa kufanyika 30 Aprili mwaka huu.Baada ya Mnyika kutoa hoja hiyo huku akizomewa na wabunge wengi wa CCM, Spika Makinda alisema kuwa suala hilo haliwezi kujadiliwa kwa sababu linafanana na lile la kuifanyia marekebisho katiba ya sasa lililokuwa limehojiwa na mbunge mwingine, kwamba yote kwa pamoja yangetolewa majibu na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda leo jioni wakati wa hotuba yake ya kuhairisha Bunge.
Hata hivyo, uamuzi wake haukukubaliwa na wabunge hao wa Ukawa ambao kwa pamoja walisimama na kuanza kupiga kelele wakisema “tunataka majibu…majibu kwanza mengine baadaye…Waziri Mkuu yupo pale atoe majibu”.
Kelele hizo ziliendelea kwa takribani dakika saba na licha ya Spika kulazimisha Katibu wa Bunge kusoma ratiba ya utaratibu unaofuata, bado hakufanikiwa na hivyo kutangaza kuliahirisha Bunge kwa muda usiojulikana hadi hapo baadaye.
Chanzo;MwanaHalisi
0 comments:
Post a Comment