Home » » MGOMO WA MADEREVA UMEISHA.

MGOMO WA MADEREVA UMEISHA.

 
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
Kuhusu suala la Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.
Miongoni mwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni kukerwa na tochi za barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.
Pia serikali imeagiza Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na Trafiki wameagizwa kulifatilia hilo.
Hali ilikuwa mbaya kwa majira ya asubuhi ambapo abiria wa mikoani na katikati ya jiji la Dar es salaam walishindwa kupata huduma ya usafiri hali iliyosababisha abiria wa mikoani kosota katika stendi ya mabasi ya Ubungo.

 


  Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kutumia mabomu ya machozi katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo kutuliza vurugu zinazofanywa na abiria pamoja na wananchi kufuatia mgomo wa madereva.

 Mgomo huo wa madereva wa mabasi na malori umeanza rasmi leo asubuhi nchi nzima na kuathiri kabisa sekta ya usafirishaji, ambapo Jijini Dar es Salaam mgomo huo pia umehusisha mabasi ya daladala.

Shuhuda wetu ameshuhudia katika neo la Ubungo bajaji na pikipiki nazo zinalazimishwa kugoma, Dereva akileta ubishi anapigwa na usafiri wake kuharibiwa.

 
Umati wa abiria wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Darajani-Ubungo huku kukiwa hakuna daladala yoyote inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa Daladala jijini Dar.
 
Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi. 
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.


Habari  toka  Morogoro  zinaarifu  kuwa  Abiria wamejazana  katika  vituo  vya  daladala, bodaboda ndo zinatoa msaada  (kwa wale wenye uwezo).
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger