Borussia Dortmund wamethibitisha kuwa Jurgen Klopp ataondoka katika
klabu hiyo ya Bundesliga mwishoni mwa msimu. Klopp, 47, ameomba
kukatisha mkataba wake ambao ulikuwa unakwenda hadi mwaka 2018.
Ameifundisha Dortmund tangu mwaka 2008 na kushinda makombe mawili ya
ligi na kucheza fainali ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2012-13. Lakini
msimu huu timu hiyo ilikuwa mkiani mwezi Januari kabla ya kupanda hadi
nafasi ya kumi, wakiwa pointi 37 nyuma ya Bayern Munich wanaoongoza
ligi. Kocha huyo amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa vya England,
ikiwemo Manchester United kabla ya kuteuliwa kwa Louis van Gaal, Arsenal
wakati ikisuasua, na baadaye mabingwa watetezi Manchester City, ambao
wamporomoka hadi nafasi ya nne, pointi 12 nyuma ya Chelsea wanaoongoza
ligi.
0 comments:
Post a Comment