Akizungumza kuelekea mchezo huo Daktari mkuu wa City, Joshua Kaseko amesema kuwa mlinzi Yusuph Abdalah ‘Sisalo’ ataukosa mchezo huo kutokana na majeraha aliyopata kwenye mcheo uliopita dhidi ya Ndanda Fc na nafasi yake itazibwa na Juma Nyosso ambaye tayari amemaliza kutumikia adhabu yake ya kutocheza mechi nane.
“Sisalo bado hali yake siyo nzuri, ni wazi hatakuwa sehemu ya kikosi kesho kwa sababu bado tunamtizamia, Juma Nyosso, amemaliza adhabu yake na kiafya yuko vizuri na imani Mwalimu Mwambusi atamjumuisha kikosini, kucheza dhidi ya Azam kunahitaji nguvu ya ziada binafsi sina wasiwasi tena na safu ya ulinzi baada ya urejeo wake” alisema.
Katika hatua nyingine mlinzi Juma Nyosso amesema yuko vizuri tayari kwa mchezo huo kwa sababu muda wote aliokuwa akitumikia adhabu alikuwa akiendelea na mazoezi.
“Niko sawa, nimekuwa nikiendelea na mazoezi muda wote niliokuwa nje ya kikosi nashukuru hayo yamepita na sasa niko tena kikosini kwa ajili ya kuipigania timu yangu, nawapongeza wenzangu wamepambana kwa nguvu zote mpaka sasa tuko kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi yaliyopita si ndwele tunaganga yajayo kwa sababu huu ndiyo wakati wa kufanya kazi” alisema.
0 comments:
Post a Comment