Uganda ilikua kwenye uchaguzi mkuu wa
kumchagua Rais na Wabunge juzi ambapo matokeo ya awali yalianza kutolewa
kuanzia jana lakini leo matokeo kamili yametolewa na Yoweri Museveni ambaye amekuwepo kwenye kiti cha Urais toka mwaka 1986 ametangazwa mshindi huku mpinzani wake mkuu ambaye ni Kizza Besigye akikataa matokeo hayo aliyoyaita ya wizi wa kura.
Kituo cha TV cha NBS kimeripoti kwamba huduma za Taxi mitaani,
mitandao ya kijamii na huduma za benki za simu za mkononi zimerejea
baada ya serikali ku
amuru juzi kila kitu kizimwe kuanzia Facebook, Twitter, Whatsapp.
Rais Museveni baadae alihojiwa na
kusema mitandao ya kijamii ilizimwa kwa muda mfupi tu na watu
hawakutakiwa kuwa na hofu sababu ilifanywa ili kuzuia upotoshaji wa
taarifa tu ambao umekua ukifanywa mara kwa mara.
Rais Museveni alipokutana na Viongozi waangalizi wa uchaguzi Mzee Obasanjo na Banda nyumbani kwa Rais eneo la Rwakitura.
0 comments:
Post a Comment