Juventus
wakiwa nyumbani dhidi ya Buyern Munich, mchezo huo umemalizika kwa timu
hizo kutoshana nguvu kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2.
Bayern
Munich ndio walioanza kuzigusa nyavu za wapinzani kwa kuandika bao la
kuongoza kupitia kwa mchezaji wao Thomas Muller dakika ya 43, muda
mchache baadaye Arjen Robben akaandika bao la pili kwa buyen Munich
katika dakika ya 55 kipindi cha pili.
Kwa
upande wao Juventus walizinduka na kuandika bao la kwanza kupitia kwa
Paulo Dybala ikiwa ni dakika ya 63 kipindi cha pili, huku Stefano
Sturaro akiandika bao la pili la kusawazisha dakika ya 76 na kuufanya
mchezo umalizike kwa sare ya kufungana bao 2-2.
Michuano
hiyo itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 2 Dynamo Kiev ikiikaribisha Man
City huko Ukraine na PSV Eindhoven wao watakuwa Wenyeji huko Uholanzi
dhidi ya Atletico Madrid.
0 comments:
Post a Comment