Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru),
imewafikisha mahakamani watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mbeya akiwamo Mkurugenzi mtendaji, Upendo Sanga kwa madai ya kuhujumu
uchumi.
Awali, Sanga alifika mahakamani hapo kusikiliza hukumu ya kesi yake iliyofunguliwa na Takukuru mwaka 2014.
Baada ya hakimu kumwaachia huru, Takukuru walimzunguka na
kumkamata tena na maofisa wake ambao walipandishwa tena kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Sarah Martin aliwasomea
mashtaka washtakiwa hao, Mweka Hazina, Hafidhi Mgagi, Mhasibu Gershom
Bwire na Sanga.
Sarah alidai kuwa washtakiwa hao walimdanganya mwajiri wao
na kujipatia fedha kwa kutumia nyaraka za kughushi na kuisababishia
Serikali hasara ya Sh4 milioni.
Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa Sanga na Mgagi kati ya
Novemba 23 hadi 28, 2012 waliidhinisha malipo ya Sh4 milioni kwa
Gershom Bwire kutengeneza vitabu 150 vya Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC).
Alidai kuwa katika shtaka la pili mshtakiwa wa tatu, Bwire
Novemba 23 na 28, 2012 alijipatia fedha isivyo halali, mali ya mwajiri.
Mwendesha mashtaka alidai kuwa washtakiwa hao wameitia hasara halmashauri kwa kujipatia Sh4 milioni.
Washtakiwa walikana mashtaka na kuachiwa kwa dhamana.
Hakimu wa mahakama hiyo, Rashid Chaungu aliahirisha kesi hiyo hadi
Februari 17.

0 comments:
Post a Comment