Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu
Joseph Kasheku (Msukuma) ameishauri serikali kuruhusu kisheria kilimo
cha Bhangi na Mirungi ili kuiwezesha kujipatia fedha za kigeni
kutokana na mauzo ya mazao hao
Mbunge huyo aliyasema hayo jana katika kikao cha 5 cha
bunge la 11 linaoendelea na vikao vyake katika ukumbi wa bunge mjini
Dodoma.
''Mheshimiwa mwenyekiti zao la mirungi na bhangi kuna nchi zinaruhusu .Mfano
mzuri mfano ni majirani zetu wa Kenya ambao ndege mbili kubwa hutua
nchini humo kuchukua mirungi na kupeleka ulaya,sasa kwa nini sisi
tusiendeleze zao hili linalopatikana Geita na maeneo ya Bunda mkoani
Mara na maeneo mengine nchini ili wananchi wanufaike kwa kuuza zao hilo
?'' Alihoji Msukuma na kuongeza;
"Kwa wasukuma kule kwetu mtu akitumia bhangi anapata
nguvu ya kulima sana hata hekari mbili lakini inakatazwa na wakati huo
huo vijana wetu tumewaruhusu kutumia viroba ambavyo huwadhoofisha sana
pengine kushinda hata bhangi, naomba tufanye utafiti upya juu ya hili.
"Wapo wenzetu humu (wabunge) wanaitumia bhangi na hakuna madhara yoyote, tena wanachangia hoja kwa ufasaha kabisa."
Baada ya hoja hiyo ya Mbunge Msukuma, Naibu Waziri Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt Khamis Kigwangalla alisimama kumjibu ambapo alisema madawa
ya kulevya aina ya bhangi na mirungi yana athari kubwa sana za kiafya na
hasa afya ya ubongo .
Kingwangalla alisema serikali kwa namna yoyote haitakubali kuruhusu au kujadili kuhalalishwa kwa madawa hayo
0 comments:
Post a Comment