Home » » KIKOSI KAMILI CHA MAN U KITAKACHO SHIRIKI EUROPA LIGI HIKI HAPA

KIKOSI KAMILI CHA MAN U KITAKACHO SHIRIKI EUROPA LIGI HIKI HAPA

KIKOSI cha Manchester United kwa ajili ya michuano ya UEFA EUROPA LIGI ambacho kimesajiliwa kwa UEFA kimeanikwa Leo na ndani yake yupo Kinda wa Miaka 17 Regan Poole.
Poole, mwenye Miaka 17 anaetoka Wales, alisainiwa na Man United kutoka Newport County mwanzoni mwa Msimu huu lakini akagubikwa na utata wa Kibali cha Uhamisho wa Kimataifa.
Lakini Juzi, Poole aliichezea Man United U-21 ikicheza na Everton na kusafisha njia kwa yeye kuwekwa kwenye Kikosi rasmi cha UEFA EUROPA LIGI.
Baadae Mwezi huu, Man United watacheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI huko Denmark na FC Midtjylland hapo Februari 18 na kurudiana Uwanjani Old Trafford Wiki moja baadae hapo Februari 25.
Kikosi ambacho kimesajiliwa kwa UEFA kwa ajili ya EUROPA LIGI kina Wachezaji 24 lakini hakina Makinda kadhaa wakiwemo Paddy McNair, Cameron Borthwick-Jackson na Andreas Pereira kwa vile wao wanakubalika kuwekwa kwenye Listi B ya Kikosi ambayo huruhusiwa idadi yeyote ya Wachezaji Chipukizi ili mradi tu wawe wamekuzwa vipaji vyao Klabuni hapo au Nchi ambayo Klabu inatoka.
Kwa vile Poole hakidhi kuwemo Listi B basi amewekwa Listi A ambay hutakiwa kuwa na Jumla ya Wachezaji 25 huku 8 ni wale ambao wamekuzwa vipaji vyao Klabuni hapo au Nchi ambayo Klabu inatoka.
MAN UNITED-Kikosi kamili kwa UEFA EUROPA LIGI:
MAKIPA: De Gea, Romero, Johnstone
MABEKI: Jones, Rojo, Smalling, Shaw, Varela, Darmian, Poole
VIUNGO: Mata, Carrick, Blind, Young, Herrera, Valencia, Fellaini, Schneiderlin, Schweinsteiger, Lingard
MAFOWADI: Rooney, Martial, Memphis, Keane
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger