Home » » vituko vya 16 bora ya Ndondo Cup Kauzu FC vs Stimtosha

vituko vya 16 bora ya Ndondo Cup Kauzu FC vs Stimtosha



Hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup 2017 inaendelea
katika Uwanja wa Kinesi uliopo Victor Wanyama Street ambapo July 20,
2017 tulishuhudia safari ya Kauzu FC kwenye michuano hiyo ikifika mwisho
baada ya kufungwa kwa penalti 4-2 dhidi ya Stimtosha.


Mgeni Rasmi katika mchezo wa Kauzu FC vs Stimtosha, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete
Mchezo huo uliingia hatua ya penalti baada ya sare ya 1-1 katika muda
wa kawaida ambapo Kauzu FC wakiwa wa mwanzo kupata bao la kuongoza
lililofungwa na Nahodha Geofrey Taita dakika ya 22 kabla ya Ally Kagawa
kuisawazishia Stimtosha dakika ya 72.


Mgeni Rasmi Ridhiwani Kikwete akikabidhi zawadi kwa Stimtosha FC baada ya kuishinda Kauzu FC kwenye mchezo wa Ndondo Cup
Inawezekana hukufika uwanjani na umepitwa na vituko vya mashabiki
mbalimbali waliojitokeza kutazama mchezo huo na ukakosa kumuona Chief wa
Kauzu baada na kabla ya kufungwa.

                                                          
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger