Hassan Dilunga akiwa ameshika mkataba wa Mtibwa Sugar baada ya kusiani miaka miwili kuhamishia huduma zake Manungu |
Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba, wamevutiwa kipaji cha kuzaliwa cha Dilunga ili kumsajili.
Katwila, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa, Taifa Stars, amesema anaamini Dilunga ni mchezaji ambaye ataisaidia timu hiyo.
Hassan Dilunga akiwa ameshika mkataba wa Mtibwa Sugar baada ya kusiani miaka miwili kuhamishia huduma zake Manungu |
Na wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Mtibwa Sugar kufika sita, baada ya awali mabingwa hao mara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, 1999 na 2000 kuwasajili kipa Shaaban Kado kutoka Mwadui, mabeki Hussein Idd kutoka Oljoro JKT, Salum Kupela Kanoni kutoka Mwadui na kiungo Suleiman Kihimb ‘Chuji’ kutoka Police Moro.
Lakini Mtibwa Sugar nayo haijaachwa salama katika dirisha hili, kwani baadhi ya wachezaji wake nao wameondoka kwenda timu nyingine, wakiwemo kipa Said Mohammed na mabeki Ally Shomary na Salim Mbonde waliohamia Simba
0 comments:
Post a Comment