Home » » ManUnited dhidi ya Real Madrid katika picha

ManUnited dhidi ya Real Madrid katika picha

Michezo

Usiku wa July 23 kuamkia July 24 ni usiku ambao mashabiki wa soka ulimwenguni waliushuhudia mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya ManUnited dhidi Real Madrid katika michuano ya International Champions Cup (ICC).

Michuano ya ICC ambayo Real Madrid na ManUnited wamekutana ni michuano mifupi ambayo hufanyika kila mwaka kama sehemu ya timu kufanya maandalizi yao ya msimu mpya wa Ligi na mashindano mbalimbali.

Mvuto wa game ya Real Madrid dhidi ya ManUnited ambayo dakika 90 zilimalizika lwa sare ya 1-1 Casemiro akiisawazishia Real Madrid goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 68 baada ya Jesse Lingard kufunga goli la uongozi kwa ManUnited dakika ya 45, wengi wameanza kuiwaza UEFA Super Cup.


Baada ya sare ya 1-1 katika dakika 90 mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo ManUnited wakapata ushindi wa penati 2-1, licha ya Real Madrid na ManUnited kucheza leo wengi wanazisubiri timu hizo katika mchezo wa UEFA Super Cup utakaochezwa August 8 2017 na unatabiriwa kuwa na mvuto zaidi.

VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)

Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger