Usiku wa July 22 2017 club ya Singida United chini ya Mkurugenzi wa club hiyo Festo Richard Sanga imekamilisha usajili wa Deus Kaseke ambaye amemaliza mkataba wake na Yanga.
Kaseke ambaye amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Singida United na muda wowote kuanzia kesho atasafiri kuelekea Mwanza kuungangana na timu iliyoweka kambi.
Winga mahiri Deus Kaseke ambaye alijiunga na Yanga akitokea Mbeya City ya jijini Mbeya, ndio anakuwa mchezaji wa mwisho kukamilisha usajili wa Singida United, kwa sasa Singida wamefunga usajili wao lakini Kigi Makassi licha ya kutotangazwa lakini wamemsajili tayari.
0 comments:
Post a Comment