Home » » Eric Bailly wa ManUnited amefungiwa na UEFA mechi 3

Eric Bailly wa ManUnited amefungiwa na UEFA mechi 3


 
Beki wa kimataifa wa Ivory Coast anayeichezea club ya Manchester United ya England Eric Bailly leo ametangazwa kufungiwa mechi tatu na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA baada ya kukutwa na hatia ya kosa alilolifanya katika mchezo wa Europa League.
Eric Bailly amefungiwa mechi tatu na UEFA kwa kosa lake alilolifanya katika mchezo wa UEFA Europa League wa Man United dhidi ya Celta Vigo la kumpiga usoni John Guidetti, hata hivyo Bailly kutokana na tukio hilo alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Leo July 24 2017 UEFA wametanga kumfungia mechi tatu Bailly kutokana na kosa hilo, hivyo kutokana na adhabu hiyo aliyopewa Bailly atakosa mchezo wa Man United dhidi ya Real Madrid wa UEFA Super Cup August 8 na atakosa mchezo wa kwanza wa Champions League hiyo baada ya kukosa mchezo wa fainali ya Europa League.
HII NI VIDEO YA TUKIO LA ERIC BAILLY DHIDI YA JOHN GUIDETTI
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger