Taarifa hiyo ambayo imerushwa na Kituo cha Channel 10 ambapo wakati wa zoezi la kuwasaka wahalifu likiendelea Kibiti leo imeripotiwa kuwa Jeshi la Polisi limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu hao.
Mkuu wa Operation hiyo Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabaas amesema tukio hilo limetokea katika eneo la Utende lililopo Kata ya Ukwiriri Wilayani Rufiji baada ya Polisi kuwatilia shaka watu watano na walipowafuatilia walikimbia na kuwashabulia Askari kwa risasi na katika majibizano Askari walifanikiwa kuwajeruhi wawili ambao walifariki njiani wakati wanapelekwa Hospital ya Taifa Muhimbili.
>>>”Baada ya kuwasimamisha watu wale hawakusimama walikimbia na kisha kufyatua risasi hewani kuelekea walipokuwa Askari. Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi watuhumiwa wawili kati ya wale watano na wakati wanapelekwa Hospitali walipoteza maisha.” – Liberatus Sabaas.
0 comments:
Post a Comment