July 19, 2017 Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu
aligoma kutoka katika chumba cha Mahakama ya wilaya Dodoma alipokuwa
akifanya shughuli zake za uwakili kwa kuhofia kukamatwa na Polisi
waliosemekana kumsubiri nje wamkamate kwa tuhuma za uchochezi.
Akiwa ndani ya Mahakama, Tundu Lissu aliongea mbele
ya Waandishi wa habari Dodoma na kusema kuwa alibaini njama za Polisi
kutaka kumkamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mke wake na kwamba
Polisi walianzia kumtafuta nyumbani Dar es salaam kabla ya kufahamu kuwa
yuko Dodoma.
Kwenye hii video hapa chini Tundu Lissu anaonekana akielezea mkasa huo…
0 comments:
Post a Comment