Home » » TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.03.2015.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.03.2015.

·      
·         MLINZI WA KAMPUNI YA KIRUMI SECIRITY SERVICE LTD AKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUIBA SILAHA BUNDUKI.

·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IBALE ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA 70.

·         WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI KINYUME CHA SHERIA.

·         WATU WANNE WAKAZI WA MTAA WA MWAKIBETE JIJINI MBEYA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA WAKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA 05.
·         JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LYESELO WILAYANI CHUNYA AKIWA AMELIMA BHANGI KWENYE SHAMBA LENYE UKUBWA WA NUSU EKARI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBEYA WILAYANI RUNGWE  ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA DONARD PETER MWAKAJONGA (62) MKAZI WA MKUNGA ALIKUTWA NJE YA NYUMBA YAKE AKIWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NJE YA NYUMBA YAKE MNAMO TAREHE 15.03.2015 MAJIRA YA SAA 18:50 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBEYA, KATA YA MKUNGA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI KIPIGO KILICHOTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA. MTUHUMIWA MMOJA AITWAYE DANIEL VENANCE (35) MKAZI WA KIJIJI CHA MBEYA AMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MLINZI WA KAMPUNI YA KIRUMI SECURITY SERVICE LTD ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ATUPELE SULUWIKE @ KIBONA (45) MKAZI WA CHIMBUYA AMEKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA SHORT - GUN  GREENER, CAR 09010503, MAKES NAMBA 09010431 YENYE SERIAL NAMBA 00097730 MALI YA MWAJILI WAKE KAMPUNI YA KIRUMI SECURITY SERVICE LTD.
MTUHUMIWA AMEKAMATWA MNAMO TAREHE 15.03.2015 MAJIRA YA SAA 10:45 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPEMBA, KATA YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
AWALI MNAMO TAREHE 14.03.2015 MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYA, KATA YA ISANDULA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA, MTUHUMIWA ALIIBA SILAHA HIYO WAKATI AKIWA LINDO ENEO LA KUEGESHA MAGARI YA KUBEBA MIZIGO MALI YA KAMPUNI YA FM ABRI NA KUELEKEA KUSIKOJULIKANA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IBALE WILAYANI KYELA AITWAYE TUMAINI SAMWEL (28) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI UJAZO WA LITA 70 ZIKIWA KWENYE MADUMU MATATU YA LITA 20 NA DUMU MOJA LA LITA 10.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.03.2015 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA IBALE, KATA YA MATEMA, TARAFA YA NTEBELA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA NA MADUMU YA POMBE HIYO AKIWA AMEYAHIFADHI ARDHINI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 
KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO WILAYANI CHUNYA AITWAYE SHIJA MAHONA (65) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI PEMBE NNE [04] ZA SWALA NA NGOZI MOJA YA CHUI. 
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.03.2015 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI HUKO KITONGOJI CHA MBUGANI, KIJIJI NA KATA YA UPENDO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MGANGA WA KIENYEJI NA HANA KIBALI CHA KUMILIKI NYARA HIZO. 
KATIKA MSAKO WA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA UPENDO AITWAYE MINDI MASHAURI (62) AMEKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI NGOZI TATU [03] ZA CHUI NA  NGOZI MOJA YA PAKAPORI. 
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.03.2015 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MWAMAPURI, KIJIJI NA KATA YA UPENDO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA HANA KIBALI CHA KUMILIKI NYARA HIZO NA ANAZITUMIA KWA MATAMBIKO YA MIFUGO YAKE. 
KATIKA MSAKO WA NNE, WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. WAZIRI MARTINE (23) 2. WILSON SHIBOKO (19) WAKAZI WA ILOMBA 3. DANIEL ATHUMAN (29) NA 4. MOSES JACKSON (27) WAKAZI WA MWAKIBETE WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05]. 
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.03.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO ENEO LA MWAKIBETE, KATA YA MWAKIBETE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA WAKIWA KWENYE KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI.
KATIKA MSAKO WA TANO, MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LYESELO WILAYANI CHUNYA AITWAYE SOPHIA SINTA (22) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA AMELIMA SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA NUSU EKARI KWA KUCHANGANYA NA ZAO LA TUMBAKU.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.03.2015 MAJIRA YA SAA 11:15 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI NA KIJIJI CHA LYESELO, KATA YA LUPA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI NYARA ZA SERIKALI BILA KIBALI KWANI KUFANYA HIVYO NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUJISHUGHULISHA NA KILIMO CHA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA NA KUACHA KULIMA/KUPANDA ZAO HARAMU LA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
 [AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBEYA WILAYANI RUNGWE AUAWA KWA KUPIGWA KUTOKANA NA KINACHODAIWA KUWA NI IMANI ZA KISHIRIKINA.

Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger