Home » » RAIS WA NIGERIA; TUTAWAMALIZA BOKO HARAM

RAIS WA NIGERIA; TUTAWAMALIZA BOKO HARAM

 
Goodluck Jonathan
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan amesema ana matumaini kwamba katika muda wa mwezi mmoja kundi la wapiganaji wa kiislamu Boko Haram halitodhibiti sehemu yoyote.

Wanamgambo hao waliokiri ushirikiano na kundi la Islamic State liliziteka sehemu kubwa ya eneo la kaskazini mashriki mwa Nigeria.

Lakini operesheni ya kieneo imesadia serikali kudhibiti miji na vijiji kadhaa.
Rais Jonathan anayewania kuchaguliwa tena katika siku nane zijazo ametetea jitihada zake za kukabiliana na ukosefu wa usalama na amesema anaamini atashinda katika uchaguzi huo.

Kiongozi huyo amesema Boko Haram linazidi kuwa dhaifu na litasamabaratishwa.
Ameeleza kwamba silaha mpya ilizopata nchi hihyo pamoja na ushirikiano na nchi jirani zimesaidia kuwasukuma wanamgambo hao nje ya miji na vijiji.

Alipoulizwa ni wapi walikokimbilia, alieleza kwamba wakati wengi wamemiminika katika mipaka ya nchi hiyo, anadhani wengine wamekimbilia katika msitu wa Sambisa ulio ngome yao kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger