Home » » MBEYA CITY KUCHEZA NA VIGOGO NDANI YA SIKU 11

MBEYA CITY KUCHEZA NA VIGOGO NDANI YA SIKU 11

 
Mbeya City itabidi ifanye kazi ya ziada kuhakikisha inabaki kwenye Ligi Kuu Bara kwani inakutana na mechi tatu ngumu ndani ya siku 11.Mbeya City iliyopoteza makali yake ya msimu uliopita kwa sasa ipo katika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 23, imebakiwa na michezo saba kati ya hiyo italazimika kupata matokeo mazuri dhidi ya Azam, Yanga na Simba ndani ya siku 11.

Mbeya City itacheza na Azam Aprili 8 kisha itaikabili Yanga Aprili 11 mechi zote zitachezwa jijini Dar es Salaam itamaliza na Simba Aprili 18 kwenye Uwanja wa Sokoine. Baada ya kumaliza mechi hizo Mbeya City itaikabili Kagera Sugar, Prisons na Polisi Morogoro mechi hizo zote zitachezwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine Mbeya.
Kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi alikiri kuwa anakabilriwa na hali ngumu kwa kuzikabili timu hizo tatu kubwa kwenye Ligi Kuu Bara, lakini wamejiandaa kwa lolote.
“Kweli si mchezo kukutana na timu tatu kubwa kwa muda mfupi na ukiangalia wao wanapambana juu kutwaa ubingwa wakati sisi huku tunatafuta nafasi ya kubaki kwenye ligi, tumejiandaa na tunaendelea
kujiandaa kwa ajili ya mechi zote zilizo mbele yetu na hatuna hofu, tutapambana na tutajua mwisho itakuaje,” alisema Mwambusi
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger