Home » » TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 06.03.2015.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 06.03.2015.

 
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWSHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KATIKA MISAKO MIWILI ILIYOFANYIKA MAENEO YA UYOLE JIJINI MBEYA.
KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE KATI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KANAN IBRAHIM (21) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA BOSS PAKETI 50.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 05.03.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
AIDHA KATIKA MSAKO WA PILI, MWANAMKE MMOJA MKAZI WA UYOLE KATI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GRACE MWAZELA (40) MFANYABIASHARA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUKAMATWA  AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI [VIROBA] AINA YA BOSS PAKETI 15 NA RIDDER PAKETI 10.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 05.03.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI/MTUMIAJI WA POMBE HIZO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI, USAMBAZAJI NA UUZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
                                                           Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger