Home »
» CHELSEA NJE UEFA,BAYERN YAUA 7-0
CHELSEA NJE UEFA,BAYERN YAUA 7-0
David Luiz akiruka juu zaidi ya Branislav Ivanovic kupiga kichwa ambacho kilimshinda kipa Courtois jana usiku
Beki wa PSG David Luiz akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la kusawazisha Dk 86
Kikosi cha kocha Jose Mourinho kimetolewa katika mashindano ya Club bingwa barani Ulaya UEFA baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na PSG katika uwanja wa Staford Brigde kwa matokeo hayo Chelsea wanaondoka katika michuano hiyo kwa magoli mengi ya kufungwa nyumbani kwani katika mchezo wa kwanza Mjini Paris,Ufaransa timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1
Kwa matokeo hayo (3-3) Chelsea wanaaga mashindano hayo maarufu barani Ulaya na Duniani kwa ujumla.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo uliocheza mjini Munich wenyeji Bayern Munich walishusha kipigo cha mwizi kwa Shakhtar Donetsk kwa kuwafunga mabao 7-0,magoli ya Bayern yalifungwa na Thomas Muller mawili moja kwa penati,Jerome Boateng,Frank Ribery,Mario Gotze,Holger Badstuber na Robert Lewandowski
Lewandowski akiteleza kufunga goli la sita
.
0 comments:
Post a Comment