Home » » HOTUBA YA RAIS MWISHO WA MWEZI FEBRUARY 2015

HOTUBA YA RAIS MWISHO WA MWEZI FEBRUARY 2015


 
 
1
HOTUBA YA MWISHO WA MWEZI FEBRUARI, 2015, YAMHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, ILIYOTOLEWA TAREHE1 MACHI, 2015Utangulizi
 Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi warehema kwa kutuwezesha kuzungumza kupitia utaratibu wetu huu mzuriwa hotuba za kila mwisho wa mwezi. Kwa mwisho wa mwezi wa Februarinina mambo matano ninayopenda kuyazungumzia.
Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura
 Ndugu Wananchi;
 Jambo la kwanza
 ni uandikishaji wa Wapiga Kura. Tarehe 24Februari, 2015 Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pindaalizindua rasmi uandikishaji wa wapiga kura ikiwa ni sehemu ya zoezi lauboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchini. Zoezi hilililizinduliwa Makambako, Mkoani Njombe na litaendelea nchini kotempaka litakapokamilika kwa mujibu wa ratiba itakayopangwa na Tume yaUchaguzi. Uandikishaji unatumia teknolojia ya kisasa ya utambuzi waalama za vidole (BVR) na macho ya mtu anayeandikishwa. Teknolojia hiiitatusaidia kuondoa kutoaminiana, manung’uniko na madai kuhusuudanganyifu katika chaguzi zetu kwamba wamepiga kura wasiostahili.Kuanza kutumika kwa teknolojia hii ni kielelezo cha utashi wa Serikalikuwa nchi yetu iwe na chaguzi zilizo huru, wazi na haki.
 Ndugu Wananchi;
Mtakumbuka kuwa, kabla ya uzinduzi wa zoezi hili, Tume ya Taifaya Uchaguzi ilifanya zoezi la majaribio ya uandikishaji wa wapiga kurakwa kutumia mashine za teknolojia hii mpya katika kata
10
 katika
 
2
Halmashauri za Kinondoni, Kilombero na Mlele kati ya tarehe 15 hadi 23Desemba, 2014. Habari njema ni kuwa, kwa kutumia mashine za BVR, idadi yawaliojiandikisha ilivuka lengo la uandikishaji kwa kipindi kilichopangwakatika Kata hizo. Katika Halmashauri ya Kilombero walioandikishwawalikia
asilimia 110.9
 ya lengo, katika Halmashauri ya Mlele uandikishajiulikia
asilimia 101
 ya lengo na katika Jimbo la Kawe, katika Halmashauriya Wilaya ya Kinondoni walioandikishwa walikuwa
asilimia 105.67
yalengo. Mafanikio haya ni ya kutia moyo pamoja na changamoto zakiufundi zilizojitokeza na zile zinazotokana na upya wa mfumo wenyewekwa watumiaji. Changamoto hizo zimefanyiwa kazi na watengenezaji wavifaa vinavyotumika katika awamu hii ya uandikishaji wa wapiga kuranchi nzima.
 Ndugu Wananchi;
Nimefarijika na taarifa kuwa zoezi la uboreshaji wa Daftari nauandikishaji wa wapiga kura limeanza vizuri Makambako. Wananchiwamejitokeza kwa wingi kuliko ilivyotarajiwa. Kati ya tarehe 23 hadi 25Februari, 2015 kwa mfano, Tume ilitegemea kuandikisha wapiga kura
9,541
lakini kutokana na mwamko wa wananchi kuwa mkubwa wamewezakuandikisha wapiga kura
13,042.
Kila kituo kilikuwa kinaandikisha kati yawapiga kura
80
 na
150
 kwa siku. Lengo la Tume ni kuandikisha wapigakura
32,000
 katika Halmashauri ya Makambako ambako kwa sikuwanatarajia kuandikisha watu
4,320
. Naambiwa kuwa hesabu za juzi na jana wameandikisha hadi wapiga kura
6,000
 kwa siku. Kwa kasi hii nakama mambo yatakwenda kama inavyotarajiwa, lengo hilo litafikiwa nahata kuvukwa.
 Ndugu Wananchi;
Hatuna budi kutoa pongeza kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwahatua hii ya kutia moyo tuliyokia katika mchakato huu. Inaondoa hofuiliyoanza kuingia miongoni mwa baadhi ya watu kuwa huenda zoezi hili
 
3
lisingefanikiwa. Tunachokitaka kwa Tume ni kuona zoezi hili linaendeleana kukamilika kama ilivyopangwa. Napenda kurudia ahadiniliyokwishaitoa kwa Tume kwamba Serikali itafanya kila linalowezekanakuiwezesha kirasilimali ili iweze kutimiza jukumu lake hilo.Nimekwishawakumbusha Hazina kuhusu umuhimu wa zoezi hilikufanikiwa kama ilivyopangwa. Hivyo basi, nimewataka wahakikishekutoa kipaumbele cha kwanza katika mgao wa fedha. Kama haifanyikinawaomba Tume waniambie mimi mwenyewe.Wito wangu kwenu, wananchi wenzangu, ni kujitokeza bila yakukosa kwenda kujiandikisha kwa mujibu wa ratiba ya uandikishaji katikamaeneo yenu kama itakavyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Msifanye ajizi maana hakutakuwepo na fursa nyingine ya kujiandikishakabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu baada ya fursa hii kupita.
 Ndugu Wananchi;
Kama ilivyoelezwa na Tume na mimi kusisitiza mara kadhaa kuwawatakaojiandikisha wakati huu ndio watakaopiga kura ya maoni kuhusuKatiba Inayopendekezwa na ndio watakaopiga kura katika Uchaguzi Mkuuwa Oktoba, mwaka huu. Vitambulisho vya zamani vya mpiga kurahavitatumika, hivyo watu wote ambao ni Watanzania na wana umri wamiaka 18 au zaidi lazima wajitokeze kuandikishwa upya. Watu pekeeambao hawatapaswa kujiandikisha tena ni wale tu walioandikishwa katikazoezi la majaribio lililofanyika katika zile kata
10
 za Halmashauri zaKinondoni, Ifakara na Mlele mwezi Desemba, 2014. Vitambulishowalivyopata ndivyo vyenyewe.
 Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii pia kuwaomba viongozi wa vyama vyasiasa, Serikali, dini na asasi za kiraia kuungana na Serikali na Tume yaUchaguzi katika kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchiwakajiandikishe. Naomba tusiwachanganye wananchi kwa kutoa taarifazisizokuwa za kweli na kuwafanya wakaacha kujiandikisha. Sisi katika
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger