Akizunguza na waandishi wa habari baada ya kufanya msako na
kuwakamata waganga hao kamanda wa polisi mkoa wa Geita SAPC Joseph Konyo
amesema wakati sasa umefika wa kuhakikisha mauaji yanayotokana na imani
potofu za kishirikina yanakomeshwa na ili kuyakomesha watu wa kwanza
kudhibitiwa ni waganga wa kienyeji wanaofanya shughuli zao pasipo
kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na nchi.
Kamanda Konyo amesema upo ushahidi wa wazi unaonyesha mahusiano ya
karibu ya mauaji haya ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi na
waganga wa kienyeji kwani ndio wahusika wanaoagiza viungo vya Albino na
ndio hao wanaopiga ramli za uongo kuonyesha kuwa vikongwe hasa wanawake
ndio wachawi.
Kamanda Konyo amesema serikali haiwezi kuvumilia waganga wa namna
hii wanaoipotosha jamii hivyo msako huu utaendeshwa katika mikoa yote
Tanzania bara ili kubaki na jamii salama isiyokuwa na vitisho vya mauaji
ya kikatili kama haya.
Baadhi ya wananchi mkoa wa Geita wameipongeza hatua ya serikali
kuanza sasa kuwachukulia hatua watuhumiwa wote wanaopatikana na tuhuma
za mauaji yanayotokana na mila potofu na ushirikina.
0 comments:
Post a Comment