Gari aina ya Toyota Hilux ambayo imegongwa na Basi la Kampuni ya Majinja likiwa linatoka Mbeya kwenda Dar. |
Mwili wa marehemu ambae hakutambulika jina lake mara moja ukiwa katika Gari ya Polisi. |
(Picha na Fahari news)
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine
zaidi ya 40 wamenusurika kifo katika ajali ya barabarani iliyotokea majira ya
saa 12:15 asubuhi njia panda ya Mafiati jijini Mbeya ikihusisha magari mawili
yaliyogongana uso kwa USO.
Ajali hiyo imehusisha basi la abiria mali ya
kampuni ya Majinja lililokuwa likielekea Dar es Salaam kutoka jijini Mbeya na
gari dogo ambalo halikufahamika Mara Moja.
kutokana na kuharibika sana ambalo dereva wake
amepoteza maisha pale pale na hakufahamika jina lake mara moja.
Pamoja na hayo shuhuda wa tukio hilo
ambaye ni mlinzi katika kituo cha Oilcom Mafiati amesema kuwa dereva wa basi la
Majinja ambaye hakufahamika kwa jina alikuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi
kitu kilicho sababisha gari kumshinda na kuparamia gari do go lililokuwa
likitokea Mwanjerwa na kuharibika kabisa.
Taarifa tuliyoipata katika eneo la tukio ni
kwamba hakuna abiria yeyote aliyejeruhiwa kutoka katika basi hilo la abiria na
mwili wa marehemu ulichukuliwa na askari kwaajili ya uchunguzi zaidi.
0 comments:
Post a Comment