WAFANYABIASHARA WAGAWANYIKA

 

Wauzaji na wamiliki wa maduka maeneo ya Mwanjelwa, Uhindini na Sido mkoani Mbeya jana waliwalaumu viongozi wao kwa kuwashinikiza kuyafunga maduka bila kutoa sababu za msingi na kuwasababishia hasara.

Wamesema tabia ya kufunga maduka inawaathiri wao na wateja badala ya Serikali inayolaumiwa.

Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao, wafanyabiashara hao walisema, viongozi wao wanawalazimisha kuyafunga maduka na kwamba atakayefungua atalipishwa Sh50,000.

“Kwa kweli nilifunga duka baada ya kushinikizwa na viongozi walionitishia kwamba watachoma moto duka nikifungua au kulipa Sh50,000,” alisema mfanyabiashara wa vifaa vya umeme.

Naye muuzaji wa bidhaa za jumla eneo la Sido, alisema tabia ya viongozi wao kuwalazimisha kufunga maduka bila maelezo ya kina inawayumbisha kiuchumi kwa vile, wateja wengi wanakosa kuchukua bidhaa zao.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Syonga Syonga hakupatikana kuelezea sababu za kulazimisha kufunga maduka hayo, lakini mjumbe wa kamati ya uongozi, aliyejitambulisha kwa jina la Amina Kyaro alisema, walifunga maduka ili kumuunga mkono Mwenyekiti wa Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja ambaye jana alifikishwa mahakamani Dodoma.

Mkoani Mwanza, jana wananchi walikosa huduma baada ya wafanyabiashara kufunga maduka yao kwa kile wanachodai ni hatua ya kumsindikiza Minja aliyefikishwa mahakamani mjini Dodoma kujibu mashtaka yanayomkabili.

Maduka mengi katikati ya jiji la Mwanza jana yalionekana kufungwa, huku baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamesimama nje na wateja wakihangaika kutafuta huduma.

Wakizungumza baadhi ya wafanyabiashara waliokutwa nje ya maduka yao, walisema wamefunga maduka yao ikiwa njia ya kumsindikiza mwenyekiti wao mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili.

Mkazi wa Nyakato, Mwanza, Rashid Mustafa alilaumu kitendo hicho na kusema hawakuwa na sababu ya kufunga maduka, tena bila kutoa taarifa kwa wateja, huku wakisababisha wananchi kukosa huduma za msingi kwani kufanya hivyo ni kuwanyanyasa kwa kuwanyima huduma.

Mkoani Kilimanjaro, pia wafanyabiashara walifunga maduka ili kuishinikiza Serikali kurekebisha mfumo wa mashine za Kieletroniki (EFD) pamoja na tozo la kodi la asilimia 100.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu tatizo hilo la mashine, baadhi ya wafanyabiashara, Grace Meela na Mbero Malya walisema kuwa mashine hizo zimekuwa zikifanya makadirio ya mauzo pekee badala ya faida, hali ambayo imekuwa ikimaliza mtaji
“Sisi tunachotaka hizo mashine zirekebishwe na tupewe bure tusiuziwe kwa kuwa hizo mashine zimekuwa zikijumlisha mauzo badala ya faida,” alisema Malya.
Walisema kilio kikubwa cha wafanyabiashara ni Serikali kurekebisha mashine hizo ikiwa ni pamoja na kuondoa tozo ya asilimia 100.


BOKO HARAM YATEKA NYARA MAMIA YA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI NIGERIA


Kutekwa nyara na Boko Haram mamia ya wanawake na watoto nchini Nigeria 

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria wamewateka nyara wanawake na watoto mia nne katika shambulio walilofanya mapema mwezi huu kwenye mji wa Damasak ulioko kilomita kadhaa kutoka kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Chad. Mji huo wa kaskazini mashariki mwa Nigeria uliokuwa ukishikiliwa na kundi la Boko Haram ulikombolewa na jeshi la nchi hiyo siku kumi zilizopita. Kwa mujibu wa mashuhuda, wanamgambo wa kundi la Boko Haram waliwaua watu 50 miongoni mwa mateka hao kabla ya kurejea nyuma kwenye ngome zao. Hadi sasa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hatima ya mateka waliosalia. Tangu kundi la kigaidi la Boko Haram lilipoanzisha mashambulio yake ndani ya ardhi ya Nigeria mwaka 2009, makumi ya maelfu ya watu wameuawa na wengine zaidi ya milioni moja wamelazimika kuyahama makaazi yao. Kutokana na kuendelea mashambulio ya kundi hilo katika miaka ya hivi karibuni, na kushindwa jeshi la Nigeria kukabiliana na mashambulio hayo, hatimaye mnamo tarehe 14 ya mwezi uliopita wa Februari, Nigeria yenyewe pamoja na Chad na Niger zilianzisha operesheni za pamoja za mashambulio dhidi ya Boko Haram. Muungano huo wa kieneo uliongeza matumaini ya kulitokomeza kundi hilo la kigaidi. Viongozi wa Nigeria wametangaza hivi karibuni kuwa miji 38 ya kaskazini mashariki imekombolewa, na magaidi wa Boko Haram wametimuliwa kutoka kwenye majimbo kadhaa waliyokuwa wakiyashikilia hususan jimbo la Borno. Huku ripoti zikieleza kuhusu kufurushwa na kurudi nyuma kundi la Boko Haram

kutoka maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na kundi hilo, kutangazwa ghafla habari ya kutekwa nyara idadi kubwa ya wanawake na watoto kumewatia hofu na mshtuko wananchi wa Nigeria. Kuibuka tena habari za shambulio na utekaji nyara uliofanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram kumejiri wakati siku chache nyuma Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria alikuwa ametangaza kwamba kundi hilo litakuwa limekwisha sambaratishwa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja. Akizungumza kwa matumaini makubwa alisema hautopindukia muda wa mwezi mmoja kabla ya Boko Haram kutimuliwa na kutolewa nje ya ardhi ya Nigeria. Rais wa Nigeria alitilia nguvu madai yake hayo kwa kuashiria kukombolewa vijiji na maeneo kadhaa katika kipindi cha wiki zilizopita kwa msaada wa majeshi ya nchi jirani, yaani Chad, Cameroon, Niger na Benin. Kwa muda mrefu, wananchi wa Nigeria wamekuwa wakimshutumu kiongozi wao huyo kwamba anaonyesha ulegevu katika kukabiliana na kundi la Boko Haram. Bali kuna hata wale waliokwenda mbali zaidi kwa kutamka kwamba Rais Jonathan anawaunga mkono nyuma ya pazia magaidi hao. Wapinzani wa serikali wanaeleza kwamba Jonathan analiunga mkono kwa siri kundi la kigaidi la Boko Haram kwa shabaha ya kuwadhoofisha Waislamu. Lakini madai yote hayo ya wapinzani yanapingwa na waungaji mkono wa kiongozi huyo. Itakumbukwa kuwa mnamo siku kadhaa nyuma, kwa mara ya kwanza, Rais wa Nigeria alikiri kwamba serikali yake haikuichukulia kwa uzito unaostahiki hatari ya kundi la Boko Haram na hivyo kuandaa suhula chache kwa ajili ya kupambana na kundi hilo. Kwa mtazamo wa wataalamu wa mambo tukio la kutekwa nyara idadi kubwa ya wanawake na watoto litaathiri nafasi ya Rais Jonathan katika uchaguzi mkuu ujao wa Nigeria. (CHANZO:Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran)

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 27,2015

 
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC_0285
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC_0295
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
. 

UFISADI;KENYATTA AWASIMAMISHA KAZI 175 NCHINI KENYA

Ufisadi:Kenyatta awasimamisha kazi maafisa wakuu serikalini 175 kufuatia tuhuma za ufisadi dhidi yao



Mawaziri 5, makatibu 6 wa kudumu na Magavana 10 wametajwa miongoni mwa maafisa 175 wa umma watakaolazimika kunga'atuka
mamlakani katika siku 60 zijazo iliuchunguzi wa kina ufanyike kuhusu madai ya ufisadi dhidi yao.
Hayo yalibainika katika ripoti iliyotolewa bungeni na rais Uhuru Kenyatta katika kikao maalum cha bunge la taifa kilichowajumuisha wabunge na maseneta.
Rais Kenyatta aliwataka maafisa wote wa umma waliotajwa katika ripoti hiyo waondoke ilituhuma zote dhidi yao zichunguzwe kwa kina na tume ya kupambana na ufisadi.
''Kwa hakika imewadia wakati ambapo serikali yangu haina budi ila kuchukua hatua mahsusi ambayo inalenga kukomesha hili zimwi la ufisadi mara moja''

UFISADI ''Ufisadi umevuka mipaka na lazima nasi tujifunge kibwebwe na kukabiliana nao''.
''Natarajia kuwa wale waliotajwa katika ripoti hii watanga'tuka mamlakani hadi pale uchunguzi utakapokamilishwa ndipo warejee afisini.'' alisema Kenyatta.
Kenyatta aliongezea kusema kuwa ''Ninamtaka kiongozi wa mashtaka ya umma kuanzisha uchunguzi mara moja kuhusiana visa vyote vilivyotajwa humu katika kipindi cha siku 60 zijazo''.
Ripoti hiyo iliyotayarishwa na tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya KACC inawadia wakati ambao kumekuwa na visa vingi vya ufisadi haswa katika serikali kuu na pia serikali za majimbo.

Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kisa kilichozua mjadala ni kile cha 'Anglo Leasing'' ambayo ilijumuisha kandarasi za idara ya Uhamiaji idara ya upelelezi na Idara ya usalama wa taifa.
Mabilioni ya fedha yalilipwa kwa wanakandarasi waliotarajiwa kuwasilisha kazi ambazo hazikuwahi kufanyika hata wa leo.
Magavana 10 kati ya 47 wametajwa katika ripoti hiyo ambayo itatangwwa rasmi siku ya jumanne katika mabunge yote mawili.
Duru zinasema kuwa Kamati nzima ya bunge inayochunguza ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma imetajwa katika ripoti hiyo.
MSAMAHA
Aidha Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kenyatta alisema''ili wakenya waweze kusonga mbele na kusahau yaliyopita kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali zilizotangulia ni wajibu wangu
kuchukua fursa hii na kuwaomba msamaha wote waliodhulumiwa kwa njia moja au nyengine.

Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Zaidi ya Wakenya 650,000 walifukuzwa makwao kufuatia vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2008 na tume maalum ya haki ukweli na maridhiano TJRC
ilipendekeza kuwa sharti serikali iombe radhi kwani fedha haziwezi kufuta machungu ya mateso ambayo wakenya wamepitia''
''Hata hivyo licha ya mapendekezo ya tume hiyo ya maridhiano,nimeagiza wizara ya fedha itenge shilingi bilioni 10 dola milioni 110, katika kipindi cha miaka
mitatu ijayo kwa ajili ya kuwafidia wale wote walioathirika''BBC

MAGAZETI LEO ALHAMISI MACHI 26,2015


 
Na Awadh Ibrahim

 

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger