Muumini apigwa risasi akiingia Kanisani Dar es Salaam



Miongoni mwa issue kadhaa zilizojadiliwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo July 24, 2017 ni pamoja na issue ya mkazi mmoja wa Ubungo Kibangu Dar es Salaam Adrian Mpande kunusurika kifo baada ya kupigwa risasi wakati akiingia Kanisani.

 

ManUnited dhidi ya Real Madrid katika picha

Michezo

Usiku wa July 23 kuamkia July 24 ni usiku ambao mashabiki wa soka ulimwenguni waliushuhudia mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya ManUnited dhidi Real Madrid katika michuano ya International Champions Cup (ICC).

Michuano ya ICC ambayo Real Madrid na ManUnited wamekutana ni michuano mifupi ambayo hufanyika kila mwaka kama sehemu ya timu kufanya maandalizi yao ya msimu mpya wa Ligi na mashindano mbalimbali.

Mvuto wa game ya Real Madrid dhidi ya ManUnited ambayo dakika 90 zilimalizika lwa sare ya 1-1 Casemiro akiisawazishia Real Madrid goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 68 baada ya Jesse Lingard kufunga goli la uongozi kwa ManUnited dakika ya 45, wengi wameanza kuiwaza UEFA Super Cup.


Baada ya sare ya 1-1 katika dakika 90 mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo ManUnited wakapata ushindi wa penati 2-1, licha ya Real Madrid na ManUnited kucheza leo wengi wanazisubiri timu hizo katika mchezo wa UEFA Super Cup utakaochezwa August 8 2017 na unatabiriwa kuwa na mvuto zaidi.

VIDEO: Gor Mahia vs Everton: Full Time 1-2 (ALL GOALS JULY 13, 2017)

NEYMAR APIGA ZOTE MBILI MAREKANI BARCA YAILAMBA JUVE 2-1

 He points up to the sky after putting demonstrating his class in front of goal as Juventus failed to cope with him
Mshambuliaji  Mbrazil, Neymar akiruka juu kwa furaha baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 15 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Juventus, tena bao la pili akifunga yeye mwenyewe dakika ya 26 usiku wa jana Uwanja wa MetLife mjini East Rutherford, New Jersey, Marekani katika mchezo wa Kombe la Mabingwa wa Kimataifa. Bao la Juve limefungwa na beki Mtaliano Giorgio Chiellini dakika ya 63 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

Baada ya taarifa za uzushi wa kifo cha King Majuto, Mboto kayaandika haya


Share


Kulikuwa na taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa kuwa muigizaji mkongwe wa Filamu na vichekesho Tanzania Amri Athuman maarufu kama King Majuto amefariki baada ya kuumwa taarifa hizo zimeelezwa kuwa sio za kweli.
Mchekeshaji maarufu Mboto Haji ambaye amefanya kazi kadhaa na Mzee Majuto ni miongoni mwa mastaa wa mwanzo kupata taarifa hizo na kulazimika kusafiri hadi Tanga nyumbani kwa mzee huyo ili kupata undani wa hali yake.
Kupitia kwenye Instagram yake leo July 23, 2017 Mboto amebainisha kwamba taarifa zilizokuwa zinasambaa kuwa King Majuto kafariki ni uzushi baada ya kufika nyumbani kwake na kumkuta angali hai.
>>>”Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu mzee majuto nimelazimika kuja kwake tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizur na sivyo kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunae.
Kwa sasa mzee ni mzima nipo nae tanga” – Mboto.


Joh Makini Ft Davido - Kata Leta (Official Music Video)

   










Rapper kutokea kundi la Weusi, Joh Makini amerudi tena kwenye TV zetu na video yake mpya iitwayo Kata Leta ambayo amemshirikisha Staa kutokea Nigeria aitwae Davido ukishaitazama video yenyewe hapa chini usiache kutuandikia comment yako umeipokeaje.
                                  

PEP AMSAINI DANILO WA REAL MADRID MIAKA MITANO MAN CITY

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akimkabidhi jezi ya timu hiyo mchezaji mpya, beki wa pembeni, Mbrazil, Danilo (kaatikati) baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 27 kutoka Real Madrid akisaini mkataba wa miaka mitano PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

EXCLUSIVE: Deus Kaseke kafunga usajili wa Singida United

 Baada ya headlines za muda mrefu za kocha wa Singida United mholanzi Hans van Pluijm kuonesha hisia zake kwa winga wa Yanga Deus Kaseke ambaye amewahi kumfundisha akiwa Yanga.


Usiku wa July 22 2017 club ya Singida United chini ya Mkurugenzi wa club hiyo Festo Richard Sanga imekamilisha usajili wa Deus Kaseke ambaye amemaliza mkataba wake na Yanga.





Kaseke ambaye amemaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Singida United na muda wowote kuanzia kesho atasafiri kuelekea Mwanza kuungangana na timu iliyoweka kambi.





Winga mahiri Deus Kaseke ambaye alijiunga na Yanga akitokea Mbeya City ya jijini Mbeya, ndio anakuwa mchezaji wa mwisho kukamilisha usajili wa Singida United, kwa sasa Singida wamefunga usajili wao lakini Kigi Makassi licha ya kutotangazwa lakini wamemsajili tayari.     

vituko vya 16 bora ya Ndondo Cup Kauzu FC vs Stimtosha



Hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup 2017 inaendelea
katika Uwanja wa Kinesi uliopo Victor Wanyama Street ambapo July 20,
2017 tulishuhudia safari ya Kauzu FC kwenye michuano hiyo ikifika mwisho
baada ya kufungwa kwa penalti 4-2 dhidi ya Stimtosha.


Mgeni Rasmi katika mchezo wa Kauzu FC vs Stimtosha, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete
Mchezo huo uliingia hatua ya penalti baada ya sare ya 1-1 katika muda
wa kawaida ambapo Kauzu FC wakiwa wa mwanzo kupata bao la kuongoza
lililofungwa na Nahodha Geofrey Taita dakika ya 22 kabla ya Ally Kagawa
kuisawazishia Stimtosha dakika ya 72.


Mgeni Rasmi Ridhiwani Kikwete akikabidhi zawadi kwa Stimtosha FC baada ya kuishinda Kauzu FC kwenye mchezo wa Ndondo Cup
Inawezekana hukufika uwanjani na umepitwa na vituko vya mashabiki
mbalimbali waliojitokeza kutazama mchezo huo na ukakosa kumuona Chief wa
Kauzu baada na kabla ya kufungwa.

                                                          

LUKAKU AFANYA KILICHOMPELEKA MAN UNITED...CITY WAFA 2-0 MAREKANI

Lukaku stole in front of Manchester City goalkeeper Ederson who had rushed off his line in the 37th minute

Mshambuliaji Mbelgiji Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia Manchester United  bao la kwanza dakika ya 37 akimalizia pasi ya 'mshikaji' wake, Mfaransa Paul Pogba katika ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu, Manchester City Alfajiri yaa leo Uwanja wa NRG mjini Houston, Texas, Marekani. Bao la pili la United lilifungwa na Marcus Rashford dakika ya 39 akimalizia pasi ya Henrikh Mkhitaryan PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

Majambazi wawili wameuawa na Polisi Kibiti…

 

Kupitia Taarifa ya Habari kwenye Televisheni za Tanzania leo July 20, 2017 zipo taarifa nyingi zimeripotiwa na moja kubwa ni kuhusu mapambano ya Polisi dhidi ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika operesheni maalum Kibiti, Pwani.
Taarifa hiyo ambayo imerushwa na Kituo cha Channel 10 ambapo wakati wa zoezi la kuwasaka wahalifu likiendelea Kibiti leo imeripotiwa kuwa Jeshi la Polisi limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu hao.
Mkuu wa Operation hiyo Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabaas amesema tukio hilo limetokea katika eneo la Utende lililopo Kata ya Ukwiriri Wilayani Rufiji baada ya Polisi kuwatilia shaka watu watano na walipowafuatilia walikimbia na kuwashabulia Askari kwa risasi na katika majibizano Askari walifanikiwa kuwajeruhi wawili ambao walifariki njiani wakati wanapelekwa Hospital ya Taifa Muhimbili.
>>>”Baada ya kuwasimamisha watu wale hawakusimama walikimbia na kisha kufyatua risasi hewani kuelekea walipokuwa Askari. Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi watuhumiwa wawili kati ya wale watano na wakati wanapelekwa Hospitali walipoteza maisha.” – Liberatus Sabaas.



 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger