Homa ya Jiji la Mbeya Derby inazidi kupanada kutokana na timu za Mbeya City na Tanzania Prison zote kutoka Jiji hapa kujipanga vizuri katika mchezo huo wa Ligi kuu Tanzania bara utakaopigwa January 25 katika Dimba la Sokoine Jiji Mbeya.
Katika historia ya Timu hizi Mbili za Jiji Mbeya, Mbeya City imekua mbabe kwa Tanzania Prison katika Mechi Mbili walizokutana katika Ligi Kuu Tanzania Bara Kwa msimu uliopita ambapo timu ya Mbeya City ilikua na Msimu wa kwanza katika ligi hiyo ambapo ilifanya Vizuri na kushika nafasi ya 3 ikiwa nyuma kwa mabingwa Azam Fc na Yanga Sc.
Katika Raundi ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania Bara Msimu uliopita Mbeya City Ilishinda kwa magoli 2-1 Tanzania Prison katika Dimba la Sokoine.Na raundi ya pili Mbeya City ikiwapigisha kwata tena Maafande hao wajela jela kwa kuwafunga 1-0.
Derby hiyo itakayochezwa January 25 mwaka huu katika dimba la Sokoine Jiji Mbeya itazikutanisha timu hizo Mbili ambazo zimeanza msimu huu vibaya,Ambapo Mbeya City hipo katika nafasi ya 11 na Ndugu zao Tanzania Prison wakibuluza mkia katika Msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa Pointi 8
Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Azam FC wamepata ushindi mnono wa magoli 3-1 Kagera sugar katika uwanja wa CCM Kirumba Jiji Mwanza.
Magoli ya mabingwa hao Wa VPL yamefungwa na Kipre Cheche 1 na Kavumbagu akitupia goli mbili huku wenyeji wao Kagera Sugar wakipata goli la kufutia macho goli,Kwa ushindi huo Azam anafikisha pointi 20 akiwa kilele tofauti ya pointi 3 dhidi ya Mtibwa Sugar na JKT Ruvu. Azam FC wanatarajiwa kuanza safari ya kurudi Jiji Dar-es-salaam alfajiri ya kesho na kuingia kambini siku hiyo hiyo ya january 21,2015.
Polisi waliwafyatulia wanafunzi gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya
Polisi
nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa
machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga
unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na
mmiliki binafsi.
Polisi hao wakiwa na Mbwa waliwatawanyta
wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka
sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na
uwanja huo.
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata
baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata
kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma
Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa
katika purukushani hilo wakati polisi walipoingilia kati na kujaribu
kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wanazua rabsha.
Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo.
Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba vijiti na kuwanyoshea.
Polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.
Walimu wa shule hio pia waliandamana wakisaidiwa na wanaharakati wa kisiasa.
Haijajulikana ambavyo mtu huyo aliweka uzio katika kiwanja hicho walichokuwa wakitumia wanafunzi kuchezea.
Wanafunzi wakigonga uzio uliokuwa umewekwa katika ardhi hio iliyonyakuliwa na mtu asiyejulikana
Baraza la jiji limesema kuwa
ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi
yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa
tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi.
Polisi mmoja alijeruhiwa katika purukushani hizo
Baadhi ya wanafunzi walibeba vijiti na kuwafukuza polisi Credit:BBC
Timu ya Mbeya City hipo jiji Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya wenyeji wao Kagera sugar.Mchezo huo unaochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba kutokana na uwanja wa Nyumbani wa Kagera sugar Uwanja wa Kaitaba kuwa katika ukarabati maalumu ambapo uwanja huo unawekewa nyasi bandia.
Mbeya City iliyopanda Daraja kwa Mafanikio msimu uliopita na kushika nafasi ya tatu katika ligi kuu Tanzania bara kesho wataingia uwanjani kwa nguvu baada ya kutoka nyumbani kwa Ushindi wa goli 1-0 Ndanda FC .
Mbeya City iliyopo katika nafasi ya 13 baada ya michezo 8 nafasi hiyo ni ya pili kutoka chini ambapo mkiani wapo ndugu zao Tanzania Prison.
Mchezo huo ni muhimu kwa kikosi hicho cha Mbeya Boys kinachonolewa na kocha Bora wa msimu uliopita Juma Mwambusi Ambapo wanatakiwa kushinda ili kufufua imani kwa mashabiki wake ambao wameonyesha uzalendo wa kutosha kwa Timu hiyo.
Mbeya City (Wana Amsha Amsha)/Wabishi Wa jiji wameanza vibaya msimu kwa kupoteza michezo
4 kati ya 8 Hali iliyopelekea kuwa nafasi mbaya katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
Wakazi wa jiji la Mbeya wana imani kubwa na timu yao Hali iliyopelekea Mashabiki wengi kusafiri mpaka Jiji Mwanza ili kuishabikia Timu hiyo.
Jumamosi Januari 17
1800 Aston Villa v Liverpool
1800 Burnley v Crystal Palace
1800 Leicester v Stoke
1800 QPR v Man United
1800 Swansea v Chelsea
1800 Tottenham v Sunderland
2030 Newcastle v Southampton
Jumapili Januari 18
1630 West Ham v Hull
1900 Man City v Arsenal
Cristiano Ronaldo ameteuliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Karne huko Nchini kwao Portugal.
Uteuzi wa Ronaldo umefanywa katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 100 ya Shirikisho la Soka la Portugal.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, nae amezoa Tuzo ya Kocha wa Karne
kwa Portugal katika Hafla hiyo hiyo iliyofanyika ndani ya Estoril
Casino, Kilomita 10 toka Jiji la Lisbon huko Nchini Portugal. Ronaldo, ambae Majuzi alizoa Tuzo ya FIFA Ballon d’Or, ikimaanisha
yeye ndie Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani huko Zurich, Uswisi, ikiwa ni
mara yake ya pili mfululizo na pia mara ya 3 kuitwaa, alifunga Bao 60
katika Mechi 61 kwa Mwaka 2014.
Kwa kuteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne, Ronaldo aliwabwaga kwa Kura Malejendari wa Portugal, Eusebio na Luis Figo.
Mwenyewe Ronaldo hakuwepo huko Portugal wakati wa Hafla hiyo kwani
alikuwa Kambini na Klabu yake Real Madrid ambayo Usiku huu inacheza Dabi
ya Jijini Madrid Uwanjani Santiago Bernabeu, ikiwa ni Marudiano ya
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey dhidi ya Atletico Madrid
ambao walishinda 2-0 katika Mechi ya kwanza waliyocheza kwao.
Kamanda wa polisi mkoa wa SINGIDA, THOBIAS SEDOYEKA
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja ameripotiwa kufariki dunia
mkoani Singida baada ya kudaiwa kunywa pombe ya kienyeji aina ya mtukulu
inayosadikiwa kuwa na sumu.
Kamanda wa polisi mkoani Singida kamishna msaidizi wa polisi
THOBIASI SEOYEKA amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema
mama mzazi wa mtoto huyo ambaye alikunywa pombe hiyo amenusurika na
amefikishwa hospitalini kwa matibabu.
Kamanda SEOYEKA amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha MSULE
wilayani IKUNGI ambapo MAGDALENA MUNA alikunywa pombe ya kienyeji aina
ya MTUKULU na kiasi kingine kumpatia na mtoto wake ili akate kiu ambaye
hata hivyo alifariki muda mfupi baada ya kunywa pombe hiyo.
Haijaweza kufahamika kama mama na mtoto huyo walikunywa pombe nyingi
kupita kiasi ama waliwekewa sumu katika pombe hiyo kwani kati ya watu
wote waliokunywa pombe hiyo MAGDALENA na Mtoto wake peke yake ndio
waliozurika.
Kwa sasa MAGDALENA amelazwa katika hospitali ya makiungu akipatiwa matibabu huku mtayarishaji wa pombe hiyo akiisaidia polisi.
Inadaiwa kuwa mila na desturi za makabila mengi ya hapa nchini
huwapatia pombe kidogo watoto wao wadogo kama njia ya kupunguza bugudha
za watoto wao husasani wanapokuwa na shughuli maalumu kama kilimo na
pengine hata wanapokuwa katika burudani.
Orodha
hiyo imeyonyesha majina ya wachezaji na viwango vya fedha ambazo
zimekuwa zikutumika kuwasajili wachezaji hao kwenda katika vilabu
Tajiri.
Lionel Messi £172.6m 2. Cristiano Ronaldo £104.3m 3. Eden
Hazard £77.6m 4. Diego Costa £65.9m 5. Paul Pogba £56.4m 6. Sergio
Aguero £51m 7. Raheem Sterling £49.4m 8. Cesc Fabregas £48.6m 9. Alexis
Sanchez £47.8m 10. Gareth Bale £47m
Mchezaji mwingine ambaye
amekuwa anahusishwa kuingia katika ushindani ni Luis Suarez, ambaye
alikuwa nyuma ya Messi na Cristiano kwa kwa kiwango cha paundi
107,000,000 kabla ya Kombe la Dunia na baada ya miezi minne.
Kikosi cha kocha Luis Van Gaal Kimelazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Aston villa katika uwanja wa Villa Park.
Aston Villa walikuwa wakwanza kupata goli dakika ya 23 kipindi cha kwanza lakini dakika ya 53 kipindi cha pili Ramadel Falco alisawazisha goli na mpaka dakika 90 zinakamilika Aston Villa 1-1 Manchester United, kwa matokeo hayo Man united wanafikisha point 32 wakiwa nafasi ya 3 nyuma ya Chelsea na Man City.