Homa ya Jiji la Mbeya Derby inazidi kupanada kutokana na timu za Mbeya City na Tanzania Prison zote kutoka Jiji hapa kujipanga vizuri katika mchezo huo wa Ligi kuu Tanzania bara utakaopigwa January 25 katika Dimba la Sokoine Jiji Mbeya.
Katika historia ya Timu hizi Mbili za Jiji Mbeya, Mbeya City imekua mbabe kwa Tanzania Prison katika Mechi Mbili walizokutana katika Ligi Kuu Tanzania Bara Kwa msimu uliopita ambapo timu ya Mbeya City ilikua na Msimu wa kwanza katika ligi hiyo ambapo ilifanya Vizuri na kushika nafasi ya 3 ikiwa nyuma kwa mabingwa Azam Fc na Yanga Sc.
Katika Raundi ya kwanza ya Ligi kuu Tanzania Bara Msimu uliopita Mbeya City Ilishinda kwa magoli 2-1 Tanzania Prison katika Dimba la Sokoine.Na raundi ya pili Mbeya City ikiwapigisha kwata tena Maafande hao wajela jela kwa kuwafunga 1-0.
Derby hiyo itakayochezwa January 25 mwaka huu katika dimba la Sokoine Jiji Mbeya itazikutanisha timu hizo Mbili ambazo zimeanza msimu huu vibaya,Ambapo Mbeya City hipo katika nafasi ya 11 na Ndugu zao Tanzania Prison wakibuluza mkia katika Msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa Pointi 8
0 comments:
Post a Comment