Home »
» MBEYA BOYS KAMILI KUWAVAA KAGERA SUGAR
MBEYA BOYS KAMILI KUWAVAA KAGERA SUGAR
Timu ya Mbeya City hipo jiji Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya wenyeji wao Kagera sugar.Mchezo huo unaochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba kutokana na uwanja wa Nyumbani wa Kagera sugar Uwanja wa Kaitaba kuwa katika ukarabati maalumu ambapo uwanja huo unawekewa nyasi bandia.
Mbeya City iliyopanda Daraja kwa Mafanikio msimu uliopita na kushika nafasi ya tatu katika ligi kuu Tanzania bara kesho wataingia uwanjani kwa nguvu baada ya kutoka nyumbani kwa Ushindi wa goli 1-0 Ndanda FC .
Mbeya City iliyopo katika nafasi ya 13 baada ya michezo 8 nafasi hiyo ni ya pili kutoka chini ambapo mkiani wapo ndugu zao Tanzania Prison.
Mchezo huo ni muhimu kwa kikosi hicho cha Mbeya Boys kinachonolewa na kocha Bora wa msimu uliopita Juma Mwambusi Ambapo wanatakiwa kushinda ili kufufua imani kwa mashabiki wake ambao wameonyesha uzalendo wa kutosha kwa Timu hiyo.
Mbeya City (Wana Amsha Amsha)/Wabishi Wa jiji wameanza vibaya msimu kwa kupoteza michezo
4 kati ya 8 Hali iliyopelekea kuwa nafasi mbaya katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.
Wakazi wa jiji la Mbeya wana imani kubwa na timu yao Hali iliyopelekea Mashabiki wengi kusafiri mpaka Jiji Mwanza ili kuishabikia Timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment