Polisi
nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa
machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga
unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na
mmiliki binafsi.
Polisi hao wakiwa na Mbwa waliwatawanyta
wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka
sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na
uwanja huo.Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.
Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo.
Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba vijiti na kuwanyoshea.
Polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.
Walimu wa shule hio pia waliandamana wakisaidiwa na wanaharakati wa kisiasa.
Haijajulikana ambavyo mtu huyo aliweka uzio katika kiwanja hicho walichokuwa wakitumia wanafunzi kuchezea.
0 comments:
Post a Comment