Kamanda wa polisi mkoa wa SINGIDA, THOBIAS SEDOYEKA
Kamanda wa polisi mkoani Singida kamishna msaidizi wa polisi THOBIASI SEOYEKA amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mama mzazi wa mtoto huyo ambaye alikunywa pombe hiyo amenusurika na amefikishwa hospitalini kwa matibabu.
Kamanda SEOYEKA amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha MSULE wilayani IKUNGI ambapo MAGDALENA MUNA alikunywa pombe ya kienyeji aina ya MTUKULU na kiasi kingine kumpatia na mtoto wake ili akate kiu ambaye hata hivyo alifariki muda mfupi baada ya kunywa pombe hiyo.
Haijaweza kufahamika kama mama na mtoto huyo walikunywa pombe nyingi kupita kiasi ama waliwekewa sumu katika pombe hiyo kwani kati ya watu wote waliokunywa pombe hiyo MAGDALENA na Mtoto wake peke yake ndio waliozurika.
Kwa sasa MAGDALENA amelazwa katika hospitali ya makiungu akipatiwa matibabu huku mtayarishaji wa pombe hiyo akiisaidia polisi.
Inadaiwa kuwa mila na desturi za makabila mengi ya hapa nchini huwapatia pombe kidogo watoto wao wadogo kama njia ya kupunguza bugudha za watoto wao husasani wanapokuwa na shughuli maalumu kama kilimo na pengine hata wanapokuwa katika burudani.
0 comments:
Post a Comment