Home » » CRISTIANO RONALDO ACHUKUA TUZO NYINGINE

CRISTIANO RONALDO ACHUKUA TUZO NYINGINE

 RONALDO-BALLONDOR2014-TROPHY 








Cristiano Ronaldo ameteuliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Karne huko Nchini kwao Portugal.

Uteuzi wa Ronaldo umefanywa katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 100 ya Shirikisho la Soka la Portugal.

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, nae amezoa Tuzo ya Kocha wa Karne kwa Portugal katika Hafla hiyo hiyo iliyofanyika ndani ya Estoril Casino, Kilomita 10 toka Jiji la Lisbon huko Nchini Portugal.
Ronaldo, ambae Majuzi alizoa Tuzo ya FIFA Ballon d’Or, ikimaanisha yeye ndie Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani huko Zurich, Uswisi, ikiwa ni mara yake ya pili mfululizo na pia mara ya 3 kuitwaa, alifunga Bao 60 katika Mechi 61 kwa Mwaka 2014.

Kwa kuteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne, Ronaldo aliwabwaga kwa Kura Malejendari wa Portugal, Eusebio na Luis Figo.

Mwenyewe Ronaldo hakuwepo huko Portugal wakati wa Hafla hiyo kwani alikuwa Kambini na Klabu yake Real Madrid ambayo Usiku huu inacheza Dabi ya Jijini Madrid Uwanjani Santiago Bernabeu, ikiwa ni Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey dhidi ya Atletico Madrid ambao walishinda 2-0 katika Mechi ya kwanza waliyocheza kwao.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger