UCHAGUZI MKUU UINGEREZA KUFANYIKA KESHO

 
Wagombea nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza

Viongozi wa vyama na wagombea wanafanya kampeni zao za mwisho kuwashawishi wapiga kura wawapigie kura kabla ya kufunguliwa uchaguzi mkuu.
Waziri Mkuu David Cameron ataahidi "kuifanya Uingereza kuwa katika njia ya mafanikio", wakati ambapo kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband ataahidi kuwa na "serikali itakayowajali kwanza wafanyakazi".
Kiongozi wa Lib Dem,Nick Clegg ataahidi hali ya utulivu.
Kura ya maoni inaonyesha hakuna chama kitakachoweza kushinda moja kwa moja kwa wingi wa viti.
Naibu mhariri wa BBC James Landale amesema wanasiasa, wapiga kura na vyombo vya habari wanajaribu kufuatilia kwa kina uchaguzi huo, na kuwafanya wengi kufuatilia kile kitakachotokea iwapo matokeo yatakuwa kinyume na matarajio yao.
"Alhamisi, huenda isiwe mwisho wa mchakato huo wa uchaguzi," amesema.
"Huenda uchaguzi huo ukaenda katika hatua ya pili baada ya kushindwa kumpata mshindi wa moja kwa moja."
Katika habari nyingine za uchaguzi mkuu:
Mgombea wa chama cha UK Independence Party (UKIP) aliondolewa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo baada ya kupigwa picha akimtishia kumpiga risasi mpinzani wake kutoka chama cha Conservative.
Kiongozi wa Labour Ed Miliband amesema haamini kama chama chake kitakopa zaidi ya ilivyokuwa mipango ya chama cha Conservative iwapo kitashinda uchaguzi.CHANZO: BBC

CHADEMA: JK AACHE ''SAFARI ZA OVYO"

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeazimia na kulaani tabia ya Rais Jakaya Kikwete kusafiri ovyo nje ya nchi wakati taifa lipo katika kipindi kigumu na matatizo makubwa ambayo yanahitaji uongozi thabiti.  
Kamati Kuu ilikutana kwa siku mbili kati ya tarehe 3 hadi 5 Mei mwaka huu, na kuitaka pia serikali kuchukua hatua za dharura kunusuru shilingi kwani athari zake ni kubwa sana kiuchumi na kijamii na kwamba zitasababisha mfumuko wa bei.
Akisoma maazimio hayo leo kwa waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa Kinondoni, Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, amesema kamati kuu vile vile ilipokea na kujadili hali halisi ya sekta ya usafirishaji nchini.
Amesema kuwa, wamebaini udhaifu mkubwa ambao upo ndani ya sekta hiyo kutokana na usimamizi dhaifu wa watu ambao walipewa dhamana kuanzia Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ambaye ameshindwa kabisa.
“Hali hiyo inasababisha sekta hiyo kukosa mwelekeo na hivyo kuleta madhara mengi kwa wananchi kutokana na ajali za kila siku kuanzia vyombo vya majini na barabarani. Kamati kuu imebaini kutokana na mgomo wa madereva wananchi wameathirika kisaikolojia na kiuchumi,”amesema.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Kamati kuu, imeazimia kuunga mkono madai ya madereva kwani ni halali na hivyo ni lazima serikali iyatekeleze madai yao yote ya muda mrefu. Amesema “kuendelea kuyapuuza ni kukubali kuendelea kuhatarisha maisha ya abiria.”
Kuhusu uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Dk. Slaa amesema kamati kuu imepokea taarifa ya kina namna ambavyo hadi sasa maandalizi ya msingi kisheria hayajafanyika. Ametaja kuwa ni mandalizi ya vifaa, fedha, kutangaza majimbo na kata mpya, kutangaza vituo na kusuasua kwa uandikishaji wapiga kura.
“Katika jambo hili, kamati kuu imeazimia kuwa uchaguzi huo lazima ufanyike Oktoba kwa mujibu wa Katiba na serikali ya CCM isijiandae kutumia kisingizio chochote kuahirisha kwa sababu uchaguzi sio jambo la dharura, bali lilijulikana miaka mitano iliyopita,” amefafanua.
CHANZO MWANAHALISI ONLINE

MGOMBEA URAIS CHADEMA KUPATIKANA AGOSTI 4


 Chadema Diaspora (Chadema or Die)
Viongozi wa Chadema wakiomba dua kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Dar es Salaam jana. Kuanzia kulia ni Makamu Mwenyekiti, Profesa Abdallah Safari, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu. Picha na Venance Nestory
Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chadema imepanga Agosti 4 kuwa siku ya kumpata mgombea wake wa urais ambaye ataingia kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Vyama vinne vilivyounda Ukawa, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja wa kuanzia ngazi ya urais, lakini kila chama kitateua mgombea wake kabla ya kukubaliana mtu atakayeungwa mkono na vyama vyote.
Ratiba iliyotolewa jana na Chadema inaonyesha kuwa chama hicho kitatumia siku 76, kuanzia Mei 18, kumaliza mchakato wa kuwapata wagombea wake wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kwa kuhitimisha na Mkutano Mkuu. Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Chadema itampata mgombea wake wa urais takriban siku 14 zaidi kulinganisha na mwaka 2010 wakati Dk Willibrod Slaa alipoteuliwa.
Kwa mujibu wa Ibara ya 7.710 (C) ya katiba ya Chadema, Mkutano Mkuu ndiyo chombo chenye mamlaka ya kumpitisha mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwaambia wanahabari jana kuwa kamati hiyo imeridhia mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu uanze ili watia nia katika maeneo mbalimbali waanze kuchukua fomu za udiwani, uwakilishi na ubunge.
Katika ratiba hiyo , chama hicho kimeyapa kipaumbele maeneo yanayoonekana kutokuwa na madiwani na wabunge, kuanza kuchukua fomu siku ya kwanza ya kazi hiyo na kuzirudisha Juni 25.
Aidha ratiba hiyo inaonyesha kuwa makada waliopo kwenye maeneo yenye madiwani watachukua na kurejesha fomu ndani ya siku 10 kuanzia Julai Mosi.
Wakati huo, maeneo yenye wabunge kwa sasa yakipatiwa siku tano za kukamilisha uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo kuanzia Julai 6 hadi 10 huku vigogo wanaounyemelea urais wakipigiwa kipenga Julai 20 hadi 25.
Mara baada ya wagombea urais kukamilisha taratibu za kinyang'anyiro, Chadema imepanga kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea ubunge Agosti 1 na 2 huku Baraza Kuu likipangwa kukutana siku inayofuata kabla ya Mkutano Mkuu kukutana Agosti, 4.
Chadema imeungana na CUF kutangaza ratiba ya kuwapata wanachama watakaowania uongozi katika Uchaguzi Mkuu ambao kikatiba unatakiwa ufanyike wiki ya mwisho ya Oktoba na kubakiza mchakato wa kumpata mgombea mmoja kila nafasi ya uongozi.
Akielezea zaidi yaliyojiri katika vikao vya kawaida vilivyofanyika Mei 3 na 4 mwaka huu, Mbowe alisema Kamati Kuu ilipokea na kujadili makubaliano yaliyofikiwa ndani ya Ukawa.
Mbowe, ambaye pia ni mbunge wa Hai, alisema kuwa kamati hiyo iliwapongeza viongozi hao kwa hatua walizofikia na kuwataka wamalize masuala machache yaliyosalia ili wawajulishe Watanzania wanaounga mkono umoja huo wajue kinachoendelea.CHANZO: MWANANCHI 

MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO WAGOMA TENA LEO





Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali  nchini, wameingia katika Mgomo tena leo kutotoa huduma hiyo kwa kile kinachodaiwa kwamba wanaitaka serikali iwasikilize madai ya mikataba yao kati yao na waajiri.
Hali ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, pamoja na watu wenye magari yao kwani baadhi ya maeneo kama jijini Mbeya magari ya watu  binafsi yamelazimishwa kupandisha abiria tena bure na baadhi ya baiskeri ya matairi matatu hali maarufu kama bajiji na pikipiki zimeendelea kutoa huduma ya usafiri kwa bei ghari zaidi hali inayopelekea wasio na kipato kutembea kwa miguu kuelekea katika shughuri zao.
hali hii imesababisha abiria wengi wa daladala kutembea kwa miguu katika jiji hapa na baadhi ya abiri a katika stendi kuu ya mabasi jiji hapa kukosa usafiri hali inayosababisha hadha kwa abiria hao ambao wamejazana katika stendi hiyo na stendi ya nane nane hali kadhalika ni hivyo hivyo.

 


RATIBA YA LIGI KUU NCHINI ENGLAND KWA WIKIEND HII HIPO HAPA

 
 
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Mei 2
1445 Leicester v Newcastle
1700 Aston Villa v Everton
1700 Liverpool v QPR
1700 Sunderland v Southampton
1700 Swansea v Stoke
1700 West Ham v Burnley
1930 Man United v West Brom
Jumapili Mei 3
1530 Chelsea v Crystal Palace
1800 Tottenham v Man City
Jumatatu Mei 4
2200 Hull v Arsenal 
 
 
 
Jumamosi Mei 9
1445 Everton v Sunderland
1700 Aston Villa v West Ham
1700 Hull v Burnley
1700 Leicester v Southampton
1700 Newcastle v West Brom
1700 Stoke v Tottenham
1930 Crystal Palace v Man United
Jumapili Mei 10
1530 Man City v QPR
1800 Chelsea v Liverpool
Jumatatu Mei 11
2200 Arsenal v Swansea
Jumamosi Mei 16
1445 Southampton v Aston Villa
1700 Burnley v Stoke
1700 QPR v Newcastle
1700 Sunderland v Leicester
1700 Tottenham v Hull
1700 West Ham v Everton
1930 Liverpool v Crystal Palace
Jumapili Mei 17
1530 Swansea v Man City
1800 Man United v Arsenal
Jumatatu Mei 18
2200 West Brom v Chelsea
Jumatano Mei 20
2145 Arsenal v Sunderland
Jumapili Mei 24
**Mechi za mwisho za Ligi
**Zote  kuanza Saa 1700
Arsenal v West Brom
Aston Villa v Burnley
Chelsea v Sunderland
Crystal Palace v Swansea
Everton v Tottenham
Hull v Man United
Leicester v QPR
Man City v Southampton
Newcastle v West Ham
Stoke v Liverpool
 
 

MANY PACQUIAO ASEMA HAYA KUELEKEA MPAMBANO WA MASUMBWI

UKAWA YAKATAA MIZENGWE YA NEC


Viongozi wa Vyama vinavyounda Umoja wa wadai Katiba ya wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe (kushoto), James Mbatia (katikati), Prof. Ibrahim Lipumba (wa pili kulia) na Dk. Emmanuel Makaidi
Viongozi wa Vyama vinavyounda Umoja wa wadai Katiba ya wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe (kushoto), James Mbatia (katikati), Prof. Ibrahim Lipumba (wa pili kulia) na Dk. Emmanuel Makaidi

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) leo vimetoa msimamo juu ya njama za kuahirisha uchaguzi mkuu unaotakiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.  

Msimamo huo wameutoa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
UKAWA imesisitiza kwamba kuahirisha Uchaguzi Mkuu ni sawa na kumuongezea  Rais Jakaya Kikwete na Chama cha Mapinduzi (CCM) muda wa kuendelea kutawala.
UKAWA imesema jaribio lolote la kuahirisha Uchaguzi Mkuu kwa kisingizio chochote kile litakuwa kinyume na Katiba ya sasa ya Tanzania na litahesabika sawa na Mapinduzi dhidi ya Katiba.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema ” Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haijaanza maandalizi yoyote kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu licha ya kwamba imebaki miezi sita tu Uchaguzi Mkuu ufanyike kwa mujibu wa Katiba”.
Lipumba amesema shughuli zinazohusiana na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu na vifaa vinavyotumika Kwa ajili yake ambavyo kwa taratibu za  miaka yote huanza kufanyika angalau mwaka mmoja na nusu kabla ya siku ya uchaguzi hazijaanza kufanyika, vifaa vinavyoohitaji havijanunuliwa na fedha kwa ajili hiyo hazijategwa hadi sasa.
Aidha, Lipumba amesema “Licha ya madai ya muda mrefu ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 imevurugwa kwa makusudi kwa kutokutenga Fedha kwa ajili hiyo katika bajeti ya serikali tangu mwaka 2012″.
“Serikali ya CCM haijatoa fedha kwa NEC kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu. Badala yake NEC imeendelea kutangaza kwamba inafanya maandalizi kwa ajili ya Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa ambayo imepitwa muda kisheria, “amesema Lipumba.
Hivyo Kwa Sheria ya Kura ya Maoni ilivyo kwa sasa, hakuna uwezekano wa Kura ya Maoni kufanyika tena bila kwanza kufanya marekebisho ya sheria hiyo.
Hadi sasa Serikali haijapeleka bungeni Muswada wa Sheria kurekebisha Sheria hiyo ili kuwezesha Kura ya Maoni.
Aidha, Mwenyekiti wa chama cha NCCR  – Mageuzi, James Mbatia amesema “kuruhusu Uchaguzi Mkuu uahirishwe kwa kisingizio chochote ni kuwazawadia wazembe na kuwaongezea mafisadi wanaolimaliza taifa kwa ufisadi muda wa kuendelea na ufisadi”.
” Watu hawa wanafahamu kuwa tumekuwa tukifanya Uchaguzi Mkuu kila baada ya miaka mitano tangu mwaka 1960. Hata mwaka 1980, miezi michache baada ya kutoka vitani dhidi ya Nduli Iddi Amin wa Uganda na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutangaza miezi 18 ya kujifunga mikanda kwa sababu ya hali mbaya ya uchumi iliyosababishwa na vita ya Uganda, hatukuahirisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo, “amesema Mbatia.
Mwenyekiti wa chama cha National League for Democracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi amesema “kubadilisha Katiba ya salsa kwa lengo la kuahirisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba sio tu kutaathiri misingi muhimu ya Katiba ya sasa, bali pia kutahatarisha amani ya nchi”.
“Tumeona kinachoendelea Burundi baada ya Raid Pierre Nkurunzinza na chama chake kuamua kuamua kujiongezea muda wa kutawala nchi hiyo. Tumeona yanayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo (DRC) baada ya Joseph Kabila kutaka kufanya hivyo. Kikwete na wanaCCM wenzake wasitake kuingiza nchi yetu katika majanga yasiyokuwa na sababu,” ameongeza Makaidi.
Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema “Tume iliwaahidi watanzania kwamba watu wote wenye sifa wataandikishwa katika Daftari la Wapiga Kura”.
“Leo Tume inapunguza muda wa siku 14 hadi siku 7 wakati tunafahamu kwamba Tume inavifaa pungufu vya kuandikisha wapiga kura. Hii ni njama ya Tume na serikali kuhakikisha wapiga kura wengi hawaandikishwi,” amesema Mbowe.
Kuhusu mgawanyo ndani ya majimbo. UKAWA imesema kati ya majimbo 239 nchi nzima, tayari wamekubaliana majimbo 227 huku majimbo 12 bado yakiwekewa vigezo kwa ajili ya kugawana.
UKAWA imekana taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu “chama cha NCCR – Mageuzi kimejitoa au kimeandika barua ya kuomba kujitoa kwenye UKAWA.

Mayweather thanks God, acknowledges the Filipinos for rallying behind wo...

Young Killer "Mungu Baba" Official Video Ft. Linah | Ommy Dimpoz | Roma

KIKWETE ATAKAPONG'ATUKA,ATAKUMBUKWA KWA LIPI?

 
 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Ingawa aliingia madarakani kwa bashasha nyingi na kauli mbiu zilizotia hamasa, lakini sasa anasema kazi ya urais ni ngumu na anatamani amalize kipindi chake ili awe mtu huru.
 

Hotuba aliyotoa Rais Jakaya Kikwete, Oktoba 2014 alipokuwa Beijing, China ni kama alianza kuwaaga Watanzania  akijiandaa kustaafu urais.
Ingawa aliingia madarakani kwa bashasha nyingi na kauli mbiu zilizotia hamasa, lakini sasa anasema kazi ya urais ni ngumu na anatamani amalize kipindi chake ili awe mtu huru.
“Ni kweli naona kama muda hauendi kwa kasi ya kutosha ili niweze kuwa raia wa kawaida na nipate muda wa kuchunga ng’ombe na mbuzi wangu, nilime mananasi yangu kwa nafasi ya kutosha,” alisema Rais Kikwete alipokuwa  mkutanoni nchini China.
Kama ilivyo ada, kila anayemaliza ngwe yake huacha kumbukumbu. Iwe mbaya au nzuri, swali ni je, yeye atakumbukwa kwa mambo gani? Je, kuna watakaolia kwa furaha kuondoka kwake au watalia kwa majonzi kwamba hawajui kesho yao?
Kikwete atakumbukwa kwa mambo makubwa na mazuri aliyowafanyia Watanzania, lakini vile vile wapo watakaomkumbuka jinsi alivyowaangusha kwa kutenda kinyume cha ahadi zake na kaulimbiu zake za Ari Mpya, Nguvu Mpya, Kasi Mpya au Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.
Watanzania wa kada mbalimbali wanazo sababu za kumkumbuka Rais Kikwete atakapong’atuka madarakani. Hii itatokana na jinsi walivyonufaika au kuumizwa kwa namna moja ama nyingine na utawala wake.
Wanawake
 
 Wanawake ni kati ya makundi katika jamii ambayo kwa namna ya pekee watamkumbuka Rais Kikwete kwa jinsi alivyothamini mchango wao na uwezo wao kiutendaji.
Ni katika awamu ya nne tangu ashike wadhifa huo, alipoongeza kasi ya kuwaamini na akawateua kwa wingi baadhi yao kuingia kwenye vyombo vya uamuzi kama uwaziri, ukuu wa mikoa na wilaya na nafasi za uwakilishi kimataifa.
Katika kipindi chake, idadi ya majaji wanawake iliongezeka, ikiwamo hata kufanikisha Anne Makinda kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu ya Spika wa Bunge. Je, atawaachia zawadi wanawake kwa kupendekeza mmoja wao kuwa mgombea urais?

Vijana

Kundi hili nalo litakuwa na kila sababu ya kuhuzunika Kikwete atakapoondoka madarakani. Hii ni kwa sababu kila alipofanya uteuzi, hakuwaacha vijana.
Tangu alipojitosa katika kinyang’anyiro cha urais kwa mara ya kwanza mwaka 1995, mkakati wake ulikuwa kuwapa vijana fursa za uongozi na aliposhinda mwaka 2005 aliwateua bila hofu katika nyadhifa mbalimbali.
Mifano ya vijana hawa ni kama January Makamba, Lazaro Nyalandu, Mwigulu Nchemba (uwaziri); Lucy Mayenga, Halima Dendegu, Wilmand Ndilu, Paul Makonda na wengineo (ukuu wa wilaya).

Wazee
 
Mbali na kuendelea kuamini busara za wazee, kila alipotaka kutangaza jambo zito au kutoa hotuba ya mwisho wa mwezi iliyotikisa nchi, alikutana na wazee ama Dar es Salaam au Dodoma, lakini vile vile wazee wamo katika nafasi mbalimbali za uongozi; uwaziri, ukuu wa wilaya na mikoa.

Wazanzibari
Rais Kikwete alijitahidi kadri ya uwezo wake kupatanisha wananchi wa Unguja na Pemba waliotofautiana kwa misingi ya siasa.
Chini ya ushawishi wake Wazanzibari walikubali kuongoza nchi kwa ushirikiano; wakaunda serikali ya Umoja wa Kitaifa. Uhasama uliondoka japokuwa kuna viashiria vya uhasama kurudi.

Wasomi
 
Hakuacha nyuma kundi la wasomi, kwani miongoni mwao ndiyo wanaoongoza wizara nyeti na taasisi mbalimbali. Aliwateua katika nafasi mbalimbali za uongozi japokuwa baadhi yao wamemwangusha.
Atakumbukwa alivyohamasisha ujenzi wa shule za sekondari kukidhi ongezeko kubwa la wanaofaulu kutoka shule za msingi na alivyojenga Chuo Kikuu cha Dodoma, upanuzi wa Chuo Kikuu Huria na vyuo vya kati.

Wanachama wa CCM
 
Tofauti na vyama vingine vya siasa, CCM wanajivunia kumpata mtu aliyekuwa kete ya ushindi kwa vipindi viwili mfululizo 2005—2010 na 2010—2015.
Watamkumbuka alivyowabeba, alivyofanyia marekebisho katiba ya chama kuwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu kutoka wilayani, alivyohuisha chama hadi kuwa na mvuto kuliko awali.
Hofu yao ni je, watampata mgombea ambaye atakuwa kete ya ushindi?

Wakulima
 
Kwa mara ya kwanza tangu Serikali ianze kuimba wimbo wa kilimo ni uti wa mgongo, safari hii wakulima na wafugaji walithaminiwa kiasi kwamba walipewa mbolea ya ruzuku, majosho na alitatua migogoro ya ardhi na malisho japo kwa kasi ndogo.

Wananchi
 
Watamkumbuka alivyowapa vyandarua, alivyojenga zahanati, vituo vya afya na alivyoongeza vifaa na majengo katika hospitali kadhaa, hususan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili; vitengo vya upasuaji wa moyo na vinginevyo.
Kigoma watamfurahia alivyojenga daraja la Mto Malagalasi pamoja na barabara ya kuunganisha na Mkoa wa Tabora; Kusini watamkumbuka alivyokamilisha daraja la Umoja; alivyoongeza vivuko na alivyofurukuta kukamilisha kipande cha kilomita 60 kutoka Ndundu hadi Somanga katika barabara ya Dar es Salaam – Mtwara iliyoanza kujengwa mwaka 1996.

Uchumi
 Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye Mkutano wa Uchumi wa Dunia WEF uliofanyika Davos
Mabadiliko ya sheria ya uwekezaji angalau yamewezesha nchi kuanza kunufaika na kodi ya uzalishaji, ingawa bado si kwa kiasi kikubwa.
Ni katika utawala wa Rais Kikwete ambapo kumekuwa na uboreshaji wa huduma za kibenki, mikopo ya saccos, uboreshaji wa njia za uchukuzi kama barabara, vivuko, reli kwa kununua vichwa na mabehewa, ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege na uwekezaji umeongezeka.

Vyama vya upinzani:
 
Miongoni mwa watakaolia kwa furaha ni wapinzani wakikumbuka kiongozi huyo alivyoshindwa kujali haki za binadamu na ushahidi ni namna Jeshi la Polisi lilivyotiririsha damu ya wapinzani wake kisiasa.
Mifano mingine ni alivyokimbilia kusuluhisha mgogoro wa Kenya huku polisi wakilaza watu kwa risasi Mtwara kufuatia mgogoro wa gesi; na Serikali yake ilivyoanzisha Operesheni Tokomeza Ujangili iliyoishia kutiririsha damu ya watu wasio na hatia kama wakulima, wafugaji na wawindaji lakini si majangili.

Wanahabari
 Cover Photo
Tasnia nzima ya habari kwa kiasi kikubwa, itamkumbuka Rais Kikwete kwa jinsi Serikali yake ilivyonyonga uhuru wa habari kwa kufungia magazeti kama Mwananchi, MwanaHalisi, Mtanzania, Kulikoni na hivi karibuni The East African na zaidi askari polisi walivyomuua mwanahabari Daudi Mwangosi chini ya utawala wake.
Kubwa zaidi kwa wanahabari ni kushindwa kwake kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya vyombo vya habari na kuondoa sheria kandamizi.

Imeandaliwa na Keneth M Mwandemange kwa msaada wa Gazeti la mwananchi
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger