Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali nchini, wameingia katika Mgomo tena leo kutotoa huduma hiyo kwa kile kinachodaiwa kwamba wanaitaka serikali iwasikilize madai ya mikataba yao kati yao na waajiri.
Hali ya
mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale
waliokuwa wakielekea mikoani, pamoja na watu wenye magari yao kwani
baadhi ya maeneo kama jijini Mbeya magari ya watu binafsi yamelazimishwa
kupandisha abiria tena bure na baadhi ya baiskeri ya matairi matatu hali maarufu kama bajiji na pikipiki zimeendelea kutoa huduma ya usafiri kwa bei ghari zaidi hali inayopelekea wasio na kipato kutembea kwa miguu kuelekea katika shughuri zao.
hali hii imesababisha abiria wengi wa daladala kutembea kwa miguu katika jiji hapa na baadhi ya abiri a katika stendi kuu ya mabasi jiji hapa kukosa usafiri hali inayosababisha hadha kwa abiria hao ambao wamejazana katika stendi hiyo na stendi ya nane nane hali kadhalika ni hivyo hivyo.
0 comments:
Post a Comment