CHADEMA:HAKUNA KULALA,HAKUNA KULA....MPAKA KIELEWEKE

 

 
Wanachama wa Chadema wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa mkakati wa ushindi katika Uchaguzi Mkuu. Mkutano huo ulifanyika Dar es Salaam jana . Picha na Said Khamis 
Na Nuzulack Dausen na Peter Elias, Mwananchi
Katika mkakati huo, chama hicho kimeigawa nchi katika kanda 10 za utekelezaji huku kikijipanga kuimarisha nguvu zaidi katika Jiji la Dar es Salaam lenye idadi kubwa ya wapigakura.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilizindua mkakati wake wa ushindi “Hakuna kulala, hakuna kula mpaka kieleweke” katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kwa kufungua mafunzo yatakayoendeshwa nchi nzima kwa viongozi wa vyama na Serikali za Mitaa.
Katika mkakati huo, chama hicho kimeigawa nchi katika kanda 10 za utekelezaji huku kikijipanga kuimarisha nguvu zaidi katika Jiji la Dar es Salaam lenye idadi kubwa ya wapigakura.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema wakati wa uzinduzi wa mkakati huo kitaifa jijini hapa kuwa watafundisha viongozi wote wa chama hicho na watangaza nia, mbinu za uongozi bora na namna ya kushinda.
Mbowe alisema mpango huo wa mafunzo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya chama kwa kuwa hawawezi kushika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa bila kuwa na viongozi bora na weledi.
Alisema Chadema kitakwenda katika kanda zote, majimbo ya kichama 242, kata 4,852, matawi 22, 749, misingi 64,803 na kuwafikia viongozi 224,287 na timu zote za mafunzo zimeshatawanyika nchi nzima.
“Tunawafundisha viongozi wetu walio tayari ndani ya chama au Serikali za Mitaa namna ya kutekeleza wajibu wao. Lakini tunawaimarisha wanaokusudia kugombea nafasi mbalimbali kuwa wagombea wazuri zaidi, kuandaa ajenda za chama na namna ya kukamata madaraka kwa kuwa safari ya kushika Dola 2015 haina kizuizi,” alisema Mbowe huku akishangiliwa.
Kuahirisha uchaguzi
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya viongozi na watia nia wa Kanda ya Pwani ya chama hicho, Mbowe aliitaka Serikali kutojaribu kabisa kuahirisha Uchaguzi Mkuu kwa sababu ya kusuasua kwa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa kutumia teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) akitishia kuwa ‘moto utawaka’.
Alisema Ukawa hawakusema chochote wakati wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilipoahirisha Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa kwa kuwa ilikuwa batili na ilianzishwa kwa masilahi ya Serikali na aliahirishwa na wao wenyewe.
Aliitaka Serikali kuharakisha uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa kuwa imesalia miezi mitatu na nusu kabla ya kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu hapo Agosti.
Alisema tarehe ya kupiga kura ambayo ni Jumapili ya Oktoba ilifahamika tangu awali kwa kuwa ni ya kikatiba lakini mpaka sasa uandikishaji unasuasua katika Mkoa wa Njombe wenye wapiga kura 340,000 ambao alisema hawafiki hata nusu ya waliopo Jimbo la Ubungo.
“Wanasubiri kama walivyofanya kwenye kuahirisha Kura ya Maoni na ili waseme ‘ndugu Watanzania kwa kuwa tumechelewa kuandikisha wapigakura tunaomba Bunge lako tukufu liongezee muda kwa Serikali ya awamu ya nne’... mtakubali?” aliwahoji wafuasi hao na kujibiwa “Hapanaaaa”.

“Serikali ikijaribu tu kuahirisha uchaguzi, nchi itawaka moto. Ikifika tarehe 25 Oktoba, Rais Jakaya Kikwete nenda Msoga (Bagamoyo) ukapumzike utuachie Ukawa na nchi yetu.”
Kuimarisha ngome Dar
Katika kile ilichoita kuimarisha ngome yenye kura nyingi, Chadema imetoa maazimio matatu kwa viongozi na wafuasi wake wa Dar es Salaam kuhakikisha inashika nafasi zote za uongozi hapo Oktoba.
Alisema jiji hili siyo tu makao makuu ya Serikali, balozi za nchi mbalimbali, au kitovu cha mapato, bali lina majimbo saba ya kwanza kwa idadi kubwa ya wapigakura kuliko mkoa wowote nchini, hivyo kusiwe na utani katika kutekeleza mikakati ya ushindi.
Mbowe, aliyesubiriwa kwa hamu tangu saa tatu asubuhi na kufika saa 6.05, alisema Jimbo la Ubungo ni la kwanza na lina wapigakura wengi kuliko hata mikoa ya Njombe na Katavi.
Akishirikiana na viongozi hao, Mbowe aliweka maazimio kuwa, Ukawa wanatakiwa kushinda majimbo yote, nafasi zote za umeya na madiwani ili kudhibiti mapato na kuleta maendeleo.
“Dhamana kubwa ya Taifa hili inawategemea wana Dar es Salaam, kazi tutakazozifanya kuanzia leo hadi siku ya uchaguzi zitasaidia nchi hii kubadilika au kuendelea kuwa na Serikali ya mabavu ya CCM,” alisema.
Alia kuzuia mpasuko
Kuhusu ugawanaji madaraka ndani ya Ukawa, Mbowe aliwataka makada hao kuvumiliana na kuzishinda changamoto zinazowakabili na kuwa Chadema na viongozi wa umoja huo wanaendelea vizuri na mipango ya ushindi.
Aliwaeleza wafuasi hao kuwa licha ya watu kuwaombea mabaya, wao hawatagombana zaidi ya kuungana kuing’oa CCM.
Alisema wanaotangaza nia wapo wengi kuliko nafasi zilizopo na atapatikana mmoja katika kila nafasi na watakaozipata, itakuwa kwa misingi ya haki na siyo dhuluma.
“Wale wote watakaokosa nafasi za kugombea ubunge na udiwani watambue kuwa vita tunavyopigana Chadema na Ukawa siyo ya kugombea madaraka. Bado wana nafasi kubwa ya kulitumikia Taifa hili kupitia Serikali yetu ya ushirika,” alisema.

Huku akishangiliwa na kuonyesha kujiamini, Mbowe aliongeza: “Tunahitaji watendaji wa Serikali, ndiyo nyinyi… msifikiri fursa ni ubunge pekee, zipo nyingi lakini zipatikane kwenye misingi ya haki, uwazi na kuheshimiana.”
Mbowe alibainisha kuwa CCM hawatakiwi kugombana huku wakitegea kusubiri mgombea wa Ukawa atangazwe ili wamtangaze wa kwao, wakifanya hivyo watasubiri sana na kwamba mgombea wa ushirika wao atatoka muda ukifika.
Ziara ya Dk Slaa
Akimkaribisha Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema Tanzania inahitaji viongozi makini watakaoweza kukiondoa CCM madarakani.
Huku akishangiliwa, Mnyika alisema lengo kuu la chama hicho ni kushika dola Oktoba mwaka huu, ndiyo maana Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa yuko Marekani kwa ajili ya kuzungumza na Watanzania waishio huko na kuimarisha uhusiano na mataifa rafiki kwa kuwa Chadema kitashika dola.
Akizungumzia ziara hiyo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando alisema Dk Slaa yuko ughaibuni kuyafuta yaliyofanywa na Serikali ya Rais Kikwete ili Ukawa iweze kuwa na uhusiano mzuri na nchi za kigeni.
Ongezeko la madiwani
Mnyika alisema kuongezeka kwa madiwani wa upinzani katika mabaraza ya madiwani na wabunge Dar es Salaam, kumeonyesha ufanisi katika kusimamia fedha za umma tofauti na hali iliyokuwa kabla ya 2010.
“Baada ya kuongezeka kwa wabunge wa upinzani katika Manispaa ya Kinondoni, mapato ya ndani ya manispaa yaliongezeka kutoka Sh7 bilioni mwaka 2010 mpaka Sh35 bilioni hivi sasa,” alisema Mnyika ambaye anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu.
Mbunge huyo alisema ufanisi unajitokeza kwa sababu viongozi wa Chadema wanafanya kazi kubwa ya kusimamia rasilimali za Taifa na kuhakikisha haziibwi.
Alisema mabadiliko yameanza kuonekana baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka jana ambao Chadema ilishinda mitaa 93 iliyopo Dar es Salaam kutoka mitatu kiliyoshinda mwaka 2009.
“Lengo letu si kuongeza idadi ya madiwani kwa ajili ya kuwa wapinzani, bali kuwa na madiwani wengi katika manispaa ya Kinondoni ili meya atoke Ukawa kuiongoza halmashauri,” alisema Mnyika huku wanachama wakimshangilia.

Uimara wa Ukawa
Marando ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, alisema Ukawa ni muungano ambao CCM haina ubavu wa kupambana nao na kwamba umedhamiria kukiondoa madarakani ili kurudisha rasilimali za nchi kwa wananchi.
Alisema wananchi wamechoshwa na dhuluma za Serikali ya CCM na kusisitiza kuwa Chadema kina viongozi wengi makini na wazalendo ambao watarejesha uhuru na haki kama alivyopigania Mwalimu Julius Nyerere.
“Wananchi wamechoshwa na miaka 50 ya CCM madarakani na mwisho wao ni Oktoba. Wanachotaka wananchi ni watu wenye nyota ya uongozi, ndiyo maana tumeanzisha mpango huu wa mafunzo,” alisema Marando.
Mwalimu na ziara ya ushindi
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema - Zanzibar, Salum Mwalimu alisema hiyo ni awamu ya pili ya kutoa mafunzo ambayo yatafanyika katika kanda za Victoria na Nyanda za Juu Kusini na Pwani na kubadilishana katika kanda zilizosalia.
Alisema wameunda vikosi vitatu vitakavyozunguka katika maeneo hayo. Kikosi cha kwanza kitakwenda Kanda ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Mara, Shinyanga na Simiyu. Kikosi hicho kitakachokuwa chini ya Mnyika kitaendelea na mafunzo katika mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita.
Kikosi cha pili kitakuwa chini Mwalimu mwenyewe na kitakwenda Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Mbeya, Rukwa, Njombe, Iringa, Morogoro na kuhitimishwa Dar es Salaam.
Mwalimu alisema kikosi cha tatu kitaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema – Tanzania Bara, Profesa Abdallah Safari na kitatoa mafunzo katika mikoa ya Pwani na Tanga.
“Kuanzia Jumamosi itakuwa ni hakuna kulala, hakuna kula, mpaka kieleweke. Ziara hii ya mafunzo itakuwa ni moto nchi nzima,” alisema Mwalimu huku wanachama wakipiga makofi.

WATU 20 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI....KAHAMA

 East Africa Television (EATV)'s photo.


Wachimbaji madini wadogo 20 waliokuwa wakichimba katika machimbo ya dhahabu ya Kalole wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi usiku wa kuamkia leo.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali peponi

18 WAFARIKI KATIKA AJALI YA HIACE ILIYOTOKEA MBEYA LEO



 


 
Watu 18 wamefariki dunia katika ajali ya hiace maeneo ya kiwira wilayani Rungwe Mkoani Mbeya na inasemekana majeruhi ni wawili gari hii ilikuwa ikiokea mbeya mjini kwenda Tukuyu.Ajali hiyo imetokea wakati Madereva wa mabasi yaendayo Wilayani Jijini Mbeya hapa kugoma kutokana na baadhi ya mabasi kukamatwa na SUMATRA kwa makosa mbalimbali na kutakiwa kulipa faini ya Tsh 200,000 kwa kila basi jambo ambalo madereva awakufikia muhafaka na kuamua kuingia katika mgomo
Hiace hiyo iliyokuwa ikitoa huduma ya Usafiri baada ya mabasi yaendayo Wilaya za Kyela,Rungwe,Mbalali na Momba kugoma mapema leo ndipo baadhi ya daladala zikaanza kutoa huduma ya usafirishaji kwenda wilayani.Mungu Azilaze Roho za marehemu pema peponi AMEN.

MKWARA WA GWAJIMA KWA KOVA WAZAA MATUNDA

 
  Mchungaji Josephat Gwajima
 
Kamanda Kova 
 
Sasa, agizo la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam la kumtaka Askofu Gwajima kuwasilisha nyaraka hizo leo limesitishwa kusubiri utatuzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka.

Dar es Salaam. Hoja za kisheria alizowasilisha Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuhusu kutakiwa kuwasilisha nyaraka 10 za utajiri na usajili wa kanisa lake polisi zimezaa matunda.
Sasa, agizo la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam la kumtaka Askofu Gwajima kuwasilisha nyaraka hizo leo limesitishwa kusubiri utatuzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka.
Wakili John Mallya anayemtetea Askofu Gwajima alilieleza gazeti hili jana usiku kuwa baada ya makubaliano na polisi mteja wake leo hatafika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kama ilivyokuwa imepangwa mpaka hoja hizo za kisheria zitakapotolewa uamuzi.
Alhamisi iliyopita, polisi ilimtaka Gwajima kuwasilisha vielelezo hivyo, lakini hatua hiyo ilipingwa na kiongozi huyo akieleza kuwa hatapeleka nyaraka yoyote iwapo jeshi hilo halitajibu barua aliyoliandikia kutaka liombe vitu hivyo kwa maandishi.
Nyaraka zilizotakiwa kuwasilishwa polisi ni hati ya usajili wa kanisa, namba ya usajili, majina ya Baraza la Wadhamini (Baraza la Kiroho), idadi ya makanisa (matawi) anayohudumia na nyaraka za helikopta ya kanisa.
Nyaraka nyingine ni; muundo wa uongozi wa kanisa, waraka wa maaskofu uliosomwa makanisa yote, nyaraka za nyumba na mali za kanisa, nyaraka kuonyesha taarifa za hesabu kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Hiari na kuambatana na mtu anayepiga picha za video kanisani hapo.
“Siwezi kuwasilisha kwa mdomo kwa kuwa hizi si mali za Gwajima… ni mali ya taasisi na si vitu vyake binafsi,” alisema wakili huyo.
Katika barua yake kwa polisi, Wakili Mallya alisema: “Tunaiomba Polisi kumwandikia rasmi mteja wetu kimaandishi nyaraka mnazozihitaji na vifungu vya sheria vinavyotumika na polisi kutaka nyaraka hizo… tutashukuru kupata hati hiyo.”
Kauli ya Kova
Mapema alipoulizwa kuhusu kitakachotokea leo, Kamanda Kova alisema: “Suala la Mchungaji Gwajima kwenda na vielelezo alivyoagizwa na Polisi siwezi kulizungumzia hadi hapo itakapotokea hakuja navyo ndipo nitakapotoa tamko langu la mwisho.
“Nitazungumziaje hili? Si hadi itokee hakuja na vielelezo na kama akija navyo halafu mimi nimeongea tofauti, nimeona italeta malumbano kati yangu na yeye na mimi sitaki ifikie huko.
“Kuna mambo mengi ya kufanya hivyo nitalitolea tamko la mwisho kwa waandishi wa habari kuhusu mchungaji Gwajima kama itatokea hivyo ili tuendelee na mambo mengine.”

Kwa msisitizo zaidi
Mallya alisema nchi inaongozwa kwa sheria, hivyo kila kitu kinatakiwa kiwe cha kisheria na kwamba wameiandikia polisi kuitaka waombe nyaraka hizo kimaandishi na kuonyesha vifungu vya sheria vinavyowaongoza kuziomba badala ya kusema kwa mdomo kwa sababu vitu hivyo ni vya kanisa na siyo vya Gwajima peke yake.
Askofu Gwajima alihojiwa na Polisi, Kanda ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kumtolea maneno makali Polycarp Kardinali Pengo baada ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kutoa tamko lililotofautiana na la viongozi wa Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu suala la Katiba.

ANGALIA ALICHOKUCHOREA KIPANYA LEO

MAGAZETI LEO ALHAMISI APRIL 16,2015


Na Awadh Ibrahim

 

UPDATE KUTOKA MKWAKWANI: MGAMBO WAIVUTA SHATI AZAM FC





                                       




Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Azam FC wametoa sare ya tatu mfululizo katika mfululizo wa michuano ya ligi kuu Tanzania baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na maafande wa jeshi la kujenga taifa JKT Mgambo katika dimba la Mkwakwani Jijini Tanga

UPDATE KUTOKA MANUNGU....MTIBWA AFUFUKIA KWA PRISON

             








 Kikosi cha wakata miwa wa Mtibwa mjini Morogoro kimefukaka tena baada ya kupata ushindi wa Goli moja kwa bila dhidi ya Tanzania Prison kutoka Jijini Mbeya katika mfurulizo wa michuano ya Ligi kuu Tanzania katika Uwanja wa Nyumbani wa Manungu Stadimu.

NYALANDU: MAJANGILI LAZIMA WASALIMU AMRI


Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikagua silaha zilizokamatwa katika hifadhi za Ruangwa, Lindi
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikagua silaha zilizokamatwa katika hifadhi za Ruangwa, Lindi 
LAZARO Nyalandu-Waziri wa Maliasili na Utalii, ametamba kuwa Serikali itapambana na ujangili hadi hapo majangili watakaposalimu amri.  
Katika mwendelezo wa vita hiyo, Nyalandu ametangaza kukamatwa kwa silaha za kivita zikiwemo bunduki za AK 47 na SMG katika Pori la Akiba la Rungwa.
Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, majangili wamevamia kwa kasi na kuwaua wanyamapori wakiwemo tembo na faru, hatua ambayo iliibua tishio la kutoweka kwa baadhi ya wanyamapori.
Silaha hizo zimekamatwa kutoka mikononi mwa majangili, ambapo katika msako huo, majangili 10 yalikamatwa kabla ya kukamilisha mipango ya kuua tembo ndani ya pori hilo.
Wakati alipoteuliwa kushika wadhifa huo, Nyalandu alitangaza vita na mtandao wa ujangili akionya kuwa kamwe hatarudi nyuma katika kulinda maliasili za taifa wakiwemo wanyamapori.
Akizungumza baada ya kukagua silaha zilizokamatwa, Nyalandu amesema serikali kamwe haitarudi nyuma hadi majangili wasalimu amri.
Alisema kukamatwa kwa shehena ya silaha hizo nyingi zikiwa na kivita, ni salamu kwa majangili kuwa serikali iko makini na inaendelea na mapambano.
Nyalandu amesema “silaha hizo zikiwemo SMG na AK47 zinatumika kwenye vita, lakini sasa majangili wanazitumia kuua tembo”.
Hata hivyo, amesema majangili hayo yalidhibitiwa kabla ya kuua tembo na kwamba, watuhumiwa 10 walitiwa mbaroni huku wananchi waishio jirani wakitoa ushirikiano mkubwa.
Amesema hakuna jangili nchini ambaye atakuwa salama iwapo hataweka silaha chini na kuwa, serikali ni lazima ishinde.
Amewaeleza askari na maofisa wa wizara yake katika Pori la Rungwa kuwa, kukamatwa kwa silaha hizo ni ishara kuwa ulinzi zaidi unapaswa kuimarishwa kwenye maeneo ya pembezoni.
Kwa mujibu wa Nyalandu, kwa sasa serikali itaelekeza nguvu zaidi katika mapori yalipo pembeni likiwemo la Rungwa.
Alisema kwa sasa askari wa wanyamapori wanaendelea kupewa mafunzo maalumu ya kijeshi kwa lengo la kuwawezesha kuwa na mbinu za kisasa zaidi za kupambana na majangili.
Alitangaza kuwa awamu ya pili ya mafunzo hayo, askari wa wanyamapori watapatiwa mafunzo ya kikomandoo zaidi ili kuwaongezea ukakamavu wa kupambana na majangili ambao wanaonekana kutumia silaha kali zaidi.
Kaimu Meneja wa Pori la Rungwa, Kwaslema Male, alimweleza Nyalandu kuwa silaha hizo zimekamatwa katika kipindi cha kuanzia Januari 2012 hadi Aprili, mwaka huu, huku idadi kubwa zikiwa zimekamatwa mwanzoni mwa mwaka huu.
Alizitaja silaha hizo kuwa ni AK 47 (2), SMG (3), Bastola (38), gobore (263), risasi za AK 47 (28), risasi za SMG (823) na misumeno ya kukatia miti kwa ajili ya mbao (197).
Male amesema “kwa sasa tumeimarisha doria katika maeneo yote ya pori hilo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi waishio jirani.

WATU 9 WAKAMATWA MSIKITINI WAKIWA NA VIFAA VYA MLIPUKO....MOROGORO

ITV Tanzania's photo.
Name:  Gaidi1.png
Views: 0
Size:  246.3 KB
 Name:  gaidi3.png
Views: 0
Size:  231.1 KB
 Name:  gaidi2.png
Views: 0
Size:  218.4 KB
  
#‎HABARIZILIZOTUFIKIA‬ HIVI PUNDE:MOROGORO
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu 9 waliokuwa wamejifungia msikitini katika eneo la Kidatu kilombero wakiwa na silaha mbali mbali na Vifaa vya milipuko ambapo katika operesheni hiyo Askari mmoja amejeruhiwa.Endelea kufuatilia taarifa zetu kufahamu zaidi
CHANZO;ITV


                                  
 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger