MAN CITY YAKAMILISHA USAJILI WA BEKI GHALI DUNIANI
Kocha Pep Guardiola (kushoto) akimkabidhi beki Benjamin Mendy jezi ya Manchester City baada ya kukamilisha uhamisho wake PICHA ZAIDI GONGA HAPA
USAJILI WA MABEKI WAPYA WA PEMBENI MANCHESTER CITY
Kyle Walker - Pauni Milioni 54
Benjamin Mendy - Pauni Milioni 52
Danilo - Pauni Milioni 27
KLABU
ya Manchester City ya England imefikisha jumla ya Pauni Milioni 133
ilizotumia kusajili mabeki wa pembeni, kufuatia kukamilisha uhamisho wa
Benjamin Mendy kutoka Monaco ya Ufaransa.
Mfaransa huyo anakuwa beki wa tatu wa pembeni kusajiliwa katika klabu hiyo, baada ya Kyle Walker na Danilo.
Mchezaji
huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa anajiunga na kikosi cha Pep Guardiola
kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 52 baada ya kwenda Los Angeles,
Marekani kufanyiwa vipimo vya afya na moja kwa moja kuungana na
wachezaji wenzake jana.
Beki
huyo mwenye umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka mitano na
kukabidhiwa jezi namba 22 atakayokuwa anatumia Uwanja wa Etihad na
anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Jumatano, ambayo itakuwa ya
kirafiki dhidi ya Real Madrid mjini LA.
CHICHARITO ASAINI MIAKA MITATU WEST HAM
Mshambuliaji
wa zamani wa Manchester United, Javier Hernandez 'Chicharito' akiwa
ameshika jezi ya West Ham United baada ya kukamilisha uhamisho wake wa
Pauni Milioni 16 kutoka Bayer Leverkusen ya Ujerumani akisaini mkataba
wa miaka mitatu na atakuwa analipwa Pauni 140,000 kwa wiki PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mtu mmoja apigwa risasi na kuuawa Mbeya.
Mwendesha Bajaj mkazi wa Njoro, Moshi ameuawa na mwili wake kufukiwa nyuma ya nyumba ya mtuhumiwa wa mauaji hayo wilayani Siha, Kilimanjaro.
Magazeti ya TZ leo July 25/2017
Eric Bailly wa ManUnited amefungiwa na UEFA mechi 3
Eric Bailly amefungiwa mechi tatu na UEFA kwa kosa lake alilolifanya katika mchezo wa UEFA Europa League wa Man United dhidi ya Celta Vigo la kumpiga usoni John Guidetti, hata hivyo Bailly kutokana na tukio hilo alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Leo July 24 2017 UEFA wametanga kumfungia mechi tatu Bailly kutokana na kosa hilo, hivyo kutokana na adhabu hiyo aliyopewa Bailly atakosa mchezo wa Man United dhidi ya Real Madrid wa UEFA Super Cup August 8 na atakosa mchezo wa kwanza wa Champions League hiyo baada ya kukosa mchezo wa fainali ya Europa League.
HII NI VIDEO YA TUKIO LA ERIC BAILLY DHIDI YA JOHN GUIDETTI
NYOTA CHELSEA WAPOZWA KWENYE MAJI YA BWAWA SINGAPORE
Wachezaji
wa Chelsea, Andreas Christensen, Victor Moses na Gary Cahill
wakifurahia kwenye bwawa la kuogelea mjini Singapore baada ya mazoezi
katika kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MTIBWA SUGAR YAMSAJILI HASSAN DILUNGA MIAKA MIWILI
![]() |
| Hassan Dilunga akiwa ameshika mkataba wa Mtibwa Sugar baada ya kusiani miaka miwili kuhamishia huduma zake Manungu |
Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba, wamevutiwa kipaji cha kuzaliwa cha Dilunga ili kumsajili.
Katwila, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya taifa, Taifa Stars, amesema anaamini Dilunga ni mchezaji ambaye ataisaidia timu hiyo.
![]() |
| Hassan Dilunga akiwa ameshika mkataba wa Mtibwa Sugar baada ya kusiani miaka miwili kuhamishia huduma zake Manungu |
Na wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Mtibwa Sugar kufika sita, baada ya awali mabingwa hao mara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, 1999 na 2000 kuwasajili kipa Shaaban Kado kutoka Mwadui, mabeki Hussein Idd kutoka Oljoro JKT, Salum Kupela Kanoni kutoka Mwadui na kiungo Suleiman Kihimb ‘Chuji’ kutoka Police Moro.
Lakini Mtibwa Sugar nayo haijaachwa salama katika dirisha hili, kwani baadhi ya wachezaji wake nao wameondoka kwenda timu nyingine, wakiwemo kipa Said Mohammed na mabeki Ally Shomary na Salim Mbonde waliohamia Simba
























































