KIKOSI KAMILI CHA MAN U KITAKACHO SHIRIKI EUROPA LIGI HIKI HAPA
KIKOSI cha Manchester United kwa
ajili ya michuano ya UEFA EUROPA LIGI ambacho kimesajiliwa kwa UEFA
kimeanikwa Leo na ndani yake yupo Kinda wa Miaka 17 Regan Poole.Poole, mwenye Miaka 17 anaetoka Wales, alisainiwa na Man United kutoka Newport County mwanzoni mwa Msimu huu lakini akagubikwa na utata wa Kibali cha Uhamisho wa Kimataifa.
Lakini Juzi, Poole aliichezea Man United U-21 ikicheza na Everton na kusafisha njia kwa yeye kuwekwa kwenye Kikosi rasmi cha UEFA EUROPA LIGI.
Baadae Mwezi huu, Man United watacheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI huko Denmark na FC Midtjylland hapo Februari 18 na kurudiana Uwanjani Old Trafford Wiki moja baadae hapo Februari 25.
Kikosi ambacho kimesajiliwa kwa UEFA kwa ajili ya EUROPA LIGI kina Wachezaji 24 lakini hakina Makinda kadhaa wakiwemo Paddy McNair, Cameron Borthwick-Jackson na Andreas Pereira kwa vile wao wanakubalika kuwekwa kwenye Listi B ya Kikosi ambayo huruhusiwa idadi yeyote ya Wachezaji Chipukizi ili mradi tu wawe wamekuzwa vipaji vyao Klabuni hapo au Nchi ambayo Klabu inatoka.
Kwa vile Poole hakidhi kuwemo Listi B basi amewekwa Listi A ambay hutakiwa kuwa na Jumla ya Wachezaji 25 huku 8 ni wale ambao wamekuzwa vipaji vyao Klabuni hapo au Nchi ambayo Klabu inatoka.
MAN UNITED-Kikosi kamili kwa UEFA EUROPA LIGI:
MAKIPA: De Gea, Romero, Johnstone
MABEKI: Jones, Rojo, Smalling, Shaw, Varela, Darmian, Poole
VIUNGO: Mata, Carrick, Blind, Young, Herrera, Valencia, Fellaini, Schneiderlin, Schweinsteiger, Lingard
MAFOWADI: Rooney, Martial, Memphis, Keane
FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: 10 BORA ZILEZILE, TANZANIA YAPANDA 1!
Belgium imebaki Nambari Wani kwenye FIFA Listi ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo huku Tanzania ikipanda Nafasi 1.10 Bora imebaki vilevile bila mabadiliko huku Mabingwa wa Dunia, Germany, wakiwa Nafasi ya 4.
Tanzania sasa ipo Nafasi ya 125 baada ya kupanda Nafasi 1 toka Mwezi uliopita walipopanda Nafasi 6.
Timu ya juu Afrika bado ni Ivory Coast lakini imeporomoka Nafasi 9 na sasa ipo Nafasi ya 28 ikifuatiwa na Cape Verde ambayo ipo Nafasi ya 33 baada ya kupanda Nafasi huku Algeria ikiwa Nafasi ya 36 baada ya kushuka Nafasi 8.
20 BORA:
1 Belgium
2 Argentina
3 Spain
4 Germany
5 Chile
6 Brazil
7 Portugal
8 Colombia
9 England
10 Austria
11 Uruguay
12 Switzerland
13 Ecuador
14 Netherlands
15 Italy
16 Romania
17 Wales
18 Croatia
19 Hungary
20 Turkey
ZEC yavitega vyama
Salum Kassim Ali, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC
Salum Kassim Ali, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC, amethibitisha kuandika alichokiita muongozo kwa vyama vilivyoshiriki uchaguzi uliofutwa 28 Oktoba akitaka vitoe tamko la kuthibitisha kama vitashiriki uchaguzi wa marudio.Salum amenukuliwa na gazeti moja akisema kwamba ameandika muongozo huo 25 Januari akitaka viwe vimetoa uhibitisho ifikapo tarehe 11 Februari.
Vyama hivyo 14 vilisimamisha mgombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi ambao siku tatu baada ya kuwa matokeo ya kura za urais yakiwa yanaendelea kutangazwa, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha aliitangaza akiwa katika udhibiti wa dola, kuufuta kwa madai kuwa umekumbwa na matatizo.
Wakati huo uchaguzi ukifutwa, Jecha alikuwa ameshatangaza matokeo ya majimbo 33 ya uchaguzi, majimbo tisa yakisubiri kutangazwa baada ya kukamilika kuhakikiwa kura zake na majimbo 12 yaliyobaki yakisubiri uhakiki.
Aidha, wakati Jecha akitangaza kufutwa kwa uchaguzi wote, tayari majimboni washindi wa uwakilishi na udiwani walishapatiwa hati zao za uthibitisho wa kushinda uchaguzi. Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi Na.11 ya mwaka 1984, hati hizo hutolewa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo na malalamiko kuhusiana na matokeo yake yatafanyiwa kazi na mahakama tu.
Hata hivyo, Chama cha Wananchi (CUF) hakijapokea barua ya Mkurugenzi wa Uchaguzi kujulishwa kuhusu kutakiwa kuthibitisha kushiriki uchaguzi wa marudio.
Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, amesema mpaka jana, hawajapokea barua hiyo ya muongozo ingawa nao walishiriki kwa kuweka mgombea urais katika uchaguzi uliofutwa.
“Pamoja na kusema kuwa hatutashiriki uchaguzi wa marudio, tunapaswa kupatiwa mawasiliano yote yanayotoka Tume kwa kuwa ni haki yetu kujua kila kinachoendelea ndani ya tume,” alisema Shehe ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT) la CUF.
Vyama vilivyopata barua ya ZEC ni ACT-Wazalendo kilichomsimamisha Khamis Iddi Lila, TADEA kilichomsimamisha Juma Ali Khatib, ADC alichoteuliwa Hamad Rashid Mohamed, AFP alichoteuliwa Said Soud Said, CCK alichoteuliwa Ali Khatib Ali, Chauma alichoteuliwa Mohamed Masoud Rashid.
Vingine ni Demokrasia Makini alichoteuliwa Tabu Mussa Juma, DP alichoteuliwa Abdalla Kombo Khamis, Jahazi Asilia alichoteuliwa Kassim Bakari Ali, NRA alichoteuliwa Seif Ali Iddi, SAU alichoteuliwa Issa Mohamed Zonga, CCM alichoteuliwa Dk. Ali Mohamed Shein na TLP alichoteuliwa Hafidh Hassan Suleiman.
Tayari baadhi ya vyama vimeshatangaza kuwa havitashiriki uchaguzi wa marudio, vingine vikiwa vinaendelea kujadiliana.
CUF kilishasema hakitashiriki uchaguzi huo kwa msimamo kuwa hakukuwa na uhalali wa kisheria wa kufutwa uchaguzi mkuu kwa vile Tume haikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo. Chama hicho kinashikilia kuitaka Tume ikamilishe kazi ya kutangaza matokeo ya kura za majimbo yaliyobakia na kumtangaza mshindi wa urais.
Kinasema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki lakini CCM ilikula njama na vyombo vya dola na kumshinikiza Jecha aufute uchaguzi huo baada ya kubaini kilishindwa.
Maalim Seif: Ondoeni shaka, nitatangazwa
Maalimu Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CUF.
Maalim Seif ametoa kauli kwenye viwanja vya Nngoma Hazingwa, Chake Chake Pemba akiwa na viongozi wa wilaya, majimbo na jumuiya za chama hicho ikiwa ni siku moja baada ya kufanya mkutano wa namna hiyo Unguja.Kiongozi huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF amesema kuwa, ukweli umedhihiri ndani na nje ya nchi na kwamba hakuna sababu ya kutotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana.
Amesema, “jumuiya na waangalizi wote wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa wameshuhudia uchaguzi huo na kujiridhisha kuwa ulikuwa huru, haki na wa uwazi na wanaendelea kushikilia msimamo wao kutaka mshindi wa uchaguzi huo atangazwe.”
Amesisitiza kuwa CUF haitoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu kauli ambayo pia imeungwa mkono na wafuasi wa chama hicho Pemba kama ilivyokuwa Unguja.
Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amemtaja Maalim Seif kuwa kiongozi aliyebobea kisiasa na anayejali maslahi ya Wazanzibari.
Katika hatua nyingine mawakilishi na madiwani wateule wa CUF kupanga kwenda mahakamani kutetea nafasi zao.
Wameeleza kwamba, kwa kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imewapa hati za ushindi baada ya kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25 Oktoba 2015, mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kupinga ushindi wao.
Hata hivyo, Maalim Seif amesema, viongozi hao waliochaguliwa na wananchi katika uchaguzi huo na kisha kupewa shahada zao, watakwenda mahakamani kutetea nafasi zao na kutoruhusu viongozi wengine wa ngazi hizo kuchaguliwa tena kwa vile wao wanavyo vielelezo vyote vya kuchaguliwa kwao.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyobandikwa katika vituo vya kupigia kura na kuthibitishwa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo, majimbo yote 18 ya uchaguzi Kisiwani Pemba yalichukuliwa na CUF, sambamba na wadi zote 32 za uchaguzi.
Mbunge Joseph Msukuma Kasheku Ataka Serikali Ihalalishe Bhangi na Mirungi Kama ilivyohalalisha Viroba

Mbunge wa Geita vijijini kwa tiketi ya CCM, ndugu
Joseph Kasheku (Msukuma) ameishauri serikali kuruhusu kisheria kilimo
cha Bhangi na Mirungi ili kuiwezesha kujipatia fedha za kigeni
kutokana na mauzo ya mazao hao
Mbunge huyo aliyasema hayo jana katika kikao cha 5 cha
bunge la 11 linaoendelea na vikao vyake katika ukumbi wa bunge mjini
Dodoma.
''Mheshimiwa mwenyekiti zao la mirungi na bhangi kuna nchi zinaruhusu .Mfano
mzuri mfano ni majirani zetu wa Kenya ambao ndege mbili kubwa hutua
nchini humo kuchukua mirungi na kupeleka ulaya,sasa kwa nini sisi
tusiendeleze zao hili linalopatikana Geita na maeneo ya Bunda mkoani
Mara na maeneo mengine nchini ili wananchi wanufaike kwa kuuza zao hilo
?'' Alihoji Msukuma na kuongeza;
"Kwa wasukuma kule kwetu mtu akitumia bhangi anapata
nguvu ya kulima sana hata hekari mbili lakini inakatazwa na wakati huo
huo vijana wetu tumewaruhusu kutumia viroba ambavyo huwadhoofisha sana
pengine kushinda hata bhangi, naomba tufanye utafiti upya juu ya hili.
"Wapo wenzetu humu (wabunge) wanaitumia bhangi na hakuna madhara yoyote, tena wanachangia hoja kwa ufasaha kabisa."
Baada ya hoja hiyo ya Mbunge Msukuma, Naibu Waziri Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt Khamis Kigwangalla alisimama kumjibu ambapo alisema madawa
ya kulevya aina ya bhangi na mirungi yana athari kubwa sana za kiafya na
hasa afya ya ubongo .
Kingwangalla alisema serikali kwa namna yoyote haitakubali kuruhusu au kujadili kuhalalishwa kwa madawa hayoAfande Sele Aungana Na Mbunge Joseph Msukuma Kuitaka Serikali Ihalalishe Matumizi Ya Bhangi

Msanii mkongwe wa hip hop nchini, Afande Sele amefunguka na
kusema serikali ihalalishe matumizi ya bangi na si kukosoa juu ya hoja
iliyotolewa na mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma.
Ikiwa imepita siku moja toka mbunge wa Geita Vijijini,
Joseph Msukuma (CCM), kusema haoni sababu ya serikali kuzuia bangi kuwa
zao la biashara kwa maana haoni madhara yake huku akidai kwamba viroba
vina madhara zaidi kuliko bangi, Afande Sele amefunguka na kusema
serikali ihalalishe matumizi ya bangi na si kukosoa juu ya hoja hiyo ya
Joseph Msukuma.
Afande Sele amedai kuwa kuna nchi ambazo tayari wao
wamehalalisha matumizi ya bangi na kuthibitisha kuwa pombe ina madhara
makubwa zaidi kuliko bangi.
"Legalize it, Don't criticize it. Korea Kaskazini,
Marekani, Mexico Uruguay na mataifa mengine ya Ulaya yamethibitisha
pombe ina madhara kuliko Cannabis Sativa" Amesema Afande Sele.
MBEYA CITY YAIMALIZA JKT BAO 2-1 KARUME
Kikosi
cha Mbeya City kimejiongezea pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu Bara
baada ya kuichapa JKT Ruvu kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Karume jijini
Dar es Salaam, leo.
Mbeya
City ilipata mabao yake yake mawili kupitia Hassan Mwasapili na Yohanna
Morris na Mussa Juma akaifungia JKT bao moja la kufutia machozi.
Kikosi
cha Mbeya City, kilisimama vema sehemu ya kiungo kikiwatumia wakongwe
Haruna Moshi 'Boban', Ramadhani Chombo 'Redondo' na kinda Raphael Alfa
na kuipa wakati mgumu JKT.
| MBEYA CITY |
| JKT RUVU |
msichana wa kitanzania azalilishwa nchini India
India ni moja kati ya
nchi ambazo vijana wengi wa kitanzania hupendelea kupelekwa na wazazi
wao kwenda kusoma, siku kadhaa nyuma ziliingia headlines kuhusu stori za
kibaguzi zinazoendelea katika nchi ya India. Inaripotiwa kuwa India mtu mweusi anabaguliwa sana.
Wiki iliyopita January 31 msichana wa kitanzania mwenye umri wa miaka 21 ambaye anasoma India
aliingia katika misukosuko ya kupigwa na kutembezwa mtupu na kundi la
watu nchini humo, wakati ambao polisi wanaripotiwa kuwa walikuwa
pembeni wakitazama tukio hilo bila kutoa msaada.
February 4 stori kutoka Bengaluru India
inaripoti kuwa polisi wamewakamata watuhumiwa watano wa tukio hilo, na
kuwafungulia mashitaka, tukio la kidhalilishaji la msichana wa
kitanzania lilifanyika baada ya usiku wa siku hiyo gari iliyokuwa
inaendeshwa na mwanafunzi raia wa Sudan anayesomea medical kumgonga mwanamke wa kihindi Sabeen Taj mwenye umri wa miaka 35 na kusababisha kifo.
Hivyo tukio la kidhalilishaji
lililofanywa na kikundi cha watu wanaoaminika kama wahindi ni kama
ishara ya kulipa kisasi cha ajali ya Sabeen Taj na mume wake Sanuallah aliyejeruhiwa.
