WANAFUNZI NCHINI KENYA WAANDAMANA KUPINGA UWEKEZAJI KATIKA ENEO LA SHULE


Polisi waliwafyatulia wanafunzi gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya


Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki binafsi.
Polisi hao wakiwa na Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo.
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.

Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma
Wanafunzi kadhaa walijeruhiwa katika purukushani hilo wakati polisi walipoingilia kati na kujaribu kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wanazua rabsha.

Baadhi yao walipelekewa hospitalini baada ya kupata majeraha madogomadogo.
Baadhi ya wanafunzi hao walikabiliana na polisi wakiwa wamebeba vijiti na kuwanyoshea.
Polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa kwa mawe.

Walimu wa shule hio pia waliandamana wakisaidiwa na wanaharakati wa kisiasa.
Haijajulikana ambavyo mtu huyo aliweka uzio katika kiwanja hicho walichokuwa wakitumia wanafunzi kuchezea.

Wanafunzi wakigonga uzio uliokuwa umewekwa katika ardhi hio iliyonyakuliwa na mtu asiyejulikana
Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi.

Polisi mmoja alijeruhiwa katika purukushani hizo
Baadhi ya wanafunzi walibeba vijiti na kuwafukuza polisi 
 
Credit:BBC 

UPDATE KUTOKA MTWARA MNYAMA AUNGURUMA

 
 
 
Kipindi cha pili kimeanza, Simba wamekianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Elius Maguli.
MAPUMZIKO:

Mapumziko kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Simba inaongoza kwa bao moja lililofungwa na Danny Sserunkuma.


Ndanda wameshambulia zaidi kuanzia dakika ya 42 huku Simba wakilinda zaidi.

MBEYA BOYS KAMILI KUWAVAA KAGERA SUGAR


Timu ya Mbeya City hipo jiji Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya wenyeji wao Kagera sugar.Mchezo huo unaochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba kutokana na uwanja wa Nyumbani wa Kagera sugar Uwanja wa Kaitaba kuwa katika ukarabati maalumu ambapo uwanja huo unawekewa nyasi bandia.




Mbeya City iliyopanda Daraja kwa Mafanikio msimu uliopita na kushika nafasi ya tatu katika ligi kuu Tanzania bara kesho wataingia uwanjani kwa nguvu baada ya kutoka nyumbani kwa Ushindi wa goli 1-0 Ndanda FC .


Mbeya City iliyopo katika nafasi ya 13 baada ya michezo 8 nafasi hiyo ni ya pili kutoka chini ambapo mkiani wapo ndugu zao Tanzania Prison.

Mchezo huo ni muhimu kwa kikosi hicho cha Mbeya Boys kinachonolewa na kocha Bora wa msimu uliopita Juma Mwambusi Ambapo wanatakiwa kushinda ili kufufua imani kwa mashabiki wake ambao wameonyesha uzalendo wa kutosha kwa Timu hiyo.

Mbeya City (Wana Amsha Amsha)/Wabishi Wa jiji wameanza vibaya msimu kwa kupoteza michezo
4 kati ya 8 Hali iliyopelekea kuwa nafasi mbaya katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara.

Wakazi wa jiji la Mbeya wana imani kubwa na timu yao Hali iliyopelekea Mashabiki wengi kusafiri mpaka Jiji Mwanza ili kuishabikia Timu hiyo.

RATIBA YA LIGI KUU NCHINI ENGLAND WIKIENDI HII HIPO HAPA

**Saa za Bongo

Jumamosi Januari 17
1800    Aston Villa v Liverpool     
1800    Burnley v Crystal Palace   
1800    Leicester v Stoke             
1800   QPR v Man United           
1800   Swansea v Chelsea          
1800   Tottenham v Sunderland  
2030   Newcastle v Southampton

Jumapili Januari 18
1630   West Ham v Hull             
1900   Man City v Arsenal             

Jumatatu Januari 19
2300   Everton v West Brom       

CITYvARSENAL


                                                                                                                                                     MSIMAMO WA LIGI HIYO BAADA YA MZUNGUKO WA 21
 BPL-TEBOJAN12










 

CRISTIANO RONALDO ACHUKUA TUZO NYINGINE

 RONALDO-BALLONDOR2014-TROPHY 








Cristiano Ronaldo ameteuliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Karne huko Nchini kwao Portugal.

Uteuzi wa Ronaldo umefanywa katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 100 ya Shirikisho la Soka la Portugal.

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, nae amezoa Tuzo ya Kocha wa Karne kwa Portugal katika Hafla hiyo hiyo iliyofanyika ndani ya Estoril Casino, Kilomita 10 toka Jiji la Lisbon huko Nchini Portugal.
Ronaldo, ambae Majuzi alizoa Tuzo ya FIFA Ballon d’Or, ikimaanisha yeye ndie Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani huko Zurich, Uswisi, ikiwa ni mara yake ya pili mfululizo na pia mara ya 3 kuitwaa, alifunga Bao 60 katika Mechi 61 kwa Mwaka 2014.

Kwa kuteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne, Ronaldo aliwabwaga kwa Kura Malejendari wa Portugal, Eusebio na Luis Figo.

Mwenyewe Ronaldo hakuwepo huko Portugal wakati wa Hafla hiyo kwani alikuwa Kambini na Klabu yake Real Madrid ambayo Usiku huu inacheza Dabi ya Jijini Madrid Uwanjani Santiago Bernabeu, ikiwa ni Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey dhidi ya Atletico Madrid ambao walishinda 2-0 katika Mechi ya kwanza waliyocheza kwao.

MTOTO WA MWAKA MMOJA AFARIKI DUNIA KWA KUNYWA POMBE YA KIENYEJI


 
Kamanda wa polisi mkoa wa SINGIDA, THOBIAS SEDOYEKA
 
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja ameripotiwa kufariki dunia mkoani Singida baada ya kudaiwa kunywa pombe ya kienyeji aina ya mtukulu inayosadikiwa kuwa na sumu.

Kamanda wa polisi mkoani Singida kamishna msaidizi wa polisi THOBIASI SEOYEKA amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mama mzazi wa mtoto huyo ambaye alikunywa pombe hiyo amenusurika na amefikishwa hospitalini kwa matibabu.

Kamanda SEOYEKA amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha MSULE wilayani IKUNGI ambapo MAGDALENA MUNA alikunywa pombe ya kienyeji aina ya MTUKULU na kiasi kingine kumpatia na mtoto wake ili akate kiu ambaye hata hivyo alifariki muda mfupi baada ya kunywa pombe hiyo.

Haijaweza kufahamika kama mama na mtoto huyo walikunywa pombe nyingi kupita kiasi ama waliwekewa sumu katika pombe hiyo kwani kati ya watu wote waliokunywa pombe hiyo MAGDALENA na Mtoto wake peke yake ndio waliozurika.

Kwa sasa MAGDALENA amelazwa katika hospitali ya makiungu akipatiwa matibabu huku mtayarishaji wa pombe hiyo akiisaidia polisi.

Inadaiwa kuwa mila na desturi za makabila mengi ya hapa nchini huwapatia pombe kidogo watoto wao wadogo kama njia ya kupunguza bugudha za watoto wao husasani wanapokuwa na shughuli maalumu kama kilimo na pengine hata wanapokuwa katika burudani.

MESSI MCHEZAJI GHALI ZAIDI DUNIANI

 
Mchezaji Lionel Messi wa Barcelona na Argentina




Orodha hiyo imeyonyesha majina ya wachezaji na viwango vya fedha ambazo zimekuwa zikutumika kuwasajili wachezaji hao kwenda katika vilabu Tajiri.


Lionel Messi £172.6m 2. Cristiano Ronaldo £104.3m 3. Eden Hazard £77.6m 4. Diego Costa £65.9m 5. Paul Pogba £56.4m 6. Sergio Aguero £51m 7. Raheem Sterling £49.4m 8. Cesc Fabregas £48.6m 9. Alexis Sanchez £47.8m 10. Gareth Bale £47m

Mchezaji mwingine ambaye amekuwa anahusishwa kuingia katika ushindani ni Luis Suarez, ambaye alikuwa nyuma ya Messi na Cristiano kwa kwa kiwango cha paundi 107,000,000 kabla ya Kombe la Dunia na baada ya miezi minne.

MATOKEO YA ASTON VILLA NA MANCHESTER UNITED YAPO HAPA



 Photo: Goal! Villa 1 United 1 (53'). Radamel Falcao's great header levels the score at Villa Park. That’s more like it!
Kikosi cha kocha Luis Van Gaal Kimelazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Aston villa katika uwanja wa Villa Park.

Photo: HT: Villa 1 United 0. The Reds have shown promise away from home but must now turn possession into goals after Christian Benteke’s opener. 

Will Louis van Gaal change tactics for the second half?

Aston Villa walikuwa wakwanza kupata goli dakika ya 23 kipindi cha kwanza lakini dakika ya 53 kipindi cha pili Ramadel Falco alisawazisha goli na mpaka dakika 90 zinakamilika Aston Villa 1-1 Manchester United, kwa matokeo hayo Man united wanafikisha point 32  wakiwa nafasi ya 3 nyuma ya Chelsea na Man City.

Izzo Bizness - Walalahoi (Official Video)

JCB Kijiti 2

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger